Redd's Miss Sinza
2013, Prisca Element (katikati) akiwa na Mshindi wa pili Happynes Maira (kulia)
na Mshindi wa tatu, Sarahy Paul, wakiwa na furaha mara baada ya kutangazwa
washindi katika shindano lao lililokuwa likishikiliwa na Redd's Miss Sinza na
Miss Tanzania 2012-2013, Brigitte Alfred.
Na Mwandishi
Wetu
MREMBO Prisca Element usiku wa kuamkia leo,
alifanikiwa kumvua taji la kwanza Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred baada ya
kufanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Sinza katika mchuano mkali uliofanyika
ukumbi wa Meeda, uliopo Sinza Mori, Dar es Salaam.
Brigitte mbali na kushikilia taji la
Redd’s Miss Tanzania ndiye pia aliyekuwa mrembo wa Redd’s Miss Tanzania, hivyo
kuvuliwa taji hilo la kwanza ni kudhihirisha kinyang’anyiro cha kumsaka mrithi
wake kimeshika kasi.
Katika shindano hilo lililokuwa kali
na la kuvutia, huku burudani ikinogeshwa na kundi la African Stars ‘Twanga
Pepeta’, nafasi ya pili ilichukuliwa na Happynes Maira na ile ya tatu akaitwaa
Sarah Paul.
Warembo wengine wawili waliofanikiwa
kuingia katika tano bora walikuwa ni Nicole Michael na Nasra Hassan, ambao
walitoa upinzani mkali katika shindano hilo lililokuwa likifuatiliwa kwa karibu
na watu wengi.
Akizungumza mara baada ya kufanikiwa
kutwaa taji hilo, Prisca alisema ana uhakika mkubwa wa kufuata nyayo za Brigitte
na kudai atahakikisha anaipigania Sinza kwa nguvu zake zote ili iweze kufanya
vyema katika Redd’s Miss Tanzania.
Brigitte alipoulizwa kuhusu shindano
hilo na kuvuliwa kwake taji, alisema anaamini kwa dhati mrembo aliyechaguliwa
atahakikisha kitongoji cha Sinza kinaendelea kufanya vizuri zaidi katika
mashindano hayo.
“Kikubwa zaidi ni kujiamini na
kufuata maelekezo unayopewa, lakini mrembo wetu naamini ana sifa zote
zinazostahili na ni matumaini yangu atasonga mbele zaidi katika hatua
inayofuata,” alisema.
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa
na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL).
No comments:
Post a Comment