Waombolezaji wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, marehemu Albert Mangwea, ulipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Raphael Gwassa)
Waombolezaji wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa msanii huyo, uwanjani hapo kwa ajili ya kwenda kuuingiza kwenye gari maalum.
Baadhi ya wasanii mbalimbali pamoja na waombolezaji wengine, wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa msanii huyo, uwanjani hapo kabla ya kuuingiza kwenye gari maalum kwa ajili ya kuupeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa.
Waombolezaji wakiwa wamelizunguka gari lililobeba jenenza lenye mwili wa marehemu Mangwea, wkabla ya kuingia barabarani kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa.
Waombolezaji wakilisukuma gari lililobeba jenenza lenye mwili wa marehemu Mangwea, wakiwa barabarani kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa. |
Umati uliojitokeza kuupokea mwili wa Mangwea, ukiwa barabarani kuusindikiza mwili huo, jijini leo.
No comments:
Post a Comment