TANGAZO


Wednesday, June 12, 2013

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecki Sadiki akabidhi nyumba kwa muathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akiwasili kwenye kijiji cha Yangeyange, Msongola kwa ajili ya kukabidhi nyumba kwa familia ya marehemu muathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, Jenifa Msigwa. Hapa akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mwendahasara Maganga. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akisalimiana na wana JKT, wajenzi wa nyumba hizo za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, mara baada ya kuwasili kijijini hapo tayari kwa ajili ya kukabidhi nyumba hiyo kwa familia hiyo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Wialaya ya Ilala na Mkoa waliofika katika hafla ya makabidhiano hayo, kijijini hapo leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akiwaeleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, alipokuwa akimweleza jambo katika hafla hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akimweleza jambo Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando,  katika hafla hiyo. 
Hii ndiyo nyumba iliyokabidhiwa kwa familia ya marehemu Jenifa Msigwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, Msongola jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Said Sadiki (katikati), katika hafla hiyo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya nyumba hiyo, Kijiji cha Yangeyange, Msongola, Dar es Salaam leo.
Wananchi wa Kijiji hicho pamoja na wageni mbalimbai waliofika katika hafla hiyo, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, wakati alipokuwa akiwahutubia kabla ya kukabidhi nyumba hiyo kwa familia hiyo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akihutubia katika hafla ya makabidhiano hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki (wa pili kulia), akipiga picha ya kumbukumbu na baba mzazi wa marehemu Jenifa Msigwa, Msafiri Msigwa (kulia kwake), mbele ya nyumba hiyo pamoja na baadhi ya viongozi aliofuatana nao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, (wa nne kushoto), akipiga picha ya kumbukumbu na familia ya marehemu Jenifa Msigwa, wakati wa makabidhiano hayo leo. Wa tatu kushoto ni baba wa marehemu Jenifa, Msafiri Msigwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki, akimkabidhi baba wa marehemu Jenifa, Msafiri Msigwa kadi ya umeme (Luku) ya nyumba hiyo pamoja na fedha keshi za kuwekea umeme.
Baba wa marehemu Jenifa, Msafiri Msigwa, akiishukuru Serikali kwa kumpatia nyumba hiyo na kueleza kuwa hiyo itakuwa ni kumbukumbu yake tosha katika maisha yake yote duniani.
Wananchi na wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo, wakishuhudia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika hafla hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akimkabidhi funguo za nyumba baba mzazi wa marehemu Jenifa Msigwa, aliyeathiriwa na mabomu ya Gongo la Mboto na baadaye kufariki, Msafiri Msigwa (kulia), wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji  cha waathirika wa mabomu hayo cha Yangeyange, Msongola, Dar es Salaam leo. Nyumba hiyo, imegharimu kiasi cha sh. 99,981,500. 
Baba wa marehemu Jenifa, Msafiri Msigwa, akifungua nyumba hiyo, mara baada ya kukabidhiwa funguo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki (kulia), katika hafla hiyo leo.

No comments:

Post a Comment