TANGAZO


Monday, June 3, 2013

Mfanyakazi wa mgodini auawa A.Kusini


Wafanyakazi 30 wa mgodini wlaiuawa mwaka jana nchini Afrika Kusini
Mwanachama wa chama cha wafanyakazi ameuawa katika mgodi wa madini ya Platinum unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin nchini Afrika Kusini, huku kukiwa na hali ya taharuki kati ya vyama hasimu vya wafanyakazi.
Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa migodini, (NUM), kimesema kuwa mauaji hayo yalifanyika karibu na mji wa Marikana, umabli wa kilomita 120 Kaskazini Magharibi mwa Johannesburg.
Polisi waliwapiga risasi, wafanyakazi 34 katika mgodi wa Marikana Agosti mwaka jana na kusababisha ghadhabu kote nchini humo.
Wakati huohuo, kampuni moja ya Uswizi imeelezea kuwa iliwafuta kazi wafanyakazi elfu moja waliofanya maandamano katika moja ya kiwanda chake wiki jana.
Migodi nchini Afrika Kusini, imekumbwa na mizozo tangu mwaka jana na kutishia imani ya waekezaji katika nchi hiyo.
"mmoja wa wanachama wetu, alishambuliwa kwa bunduki katika ofisi yetu ya Lonmin Magharibi mwa nchi,'' alisema msemaji Lesiba Seshoka.
Bwana Seshoka alisema kuwa hajui nani aliyefanya mauaji hayo.
Takriban watu 50 waliuawa mwaka jana katika migomo iliyokumbwa na ghasia kati ya vyama hasimu vya wafanyakazi na kile cha wajenzi.
Kundi moja linatuhumu lengine kwa kuwa na uhusiano wa karibu sana na wasimamizi wakuu wa serikali , tuhuma iliyokanushwa vikali.

No comments:

Post a Comment