Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, akitoa maelezo mafupi ya Rasimu Katiba Mpya kabla ya kuzinduzinduliwa rasmi na Makamu Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk wa bayana.blogspot)
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, akitoa maelezo mafupi ya Rasimu Katiba Mpya kabla ya kuzinduzinduliwa rasmi na Makamu Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza maelezo ya Rasimu ya Katiba mpya, yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu, Joseph Warioba.
Makamu Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati hafla ya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba mpya, Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati hafla ya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba mpya, Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Anjela Kairuki (kushoto), Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari (kulia), Wanasheria Wakuu wa Tanzania, Jaji Werema (wa pili kushoto) na wa Zanzibar, Othman Masoud Othman (wa pili kulia), wakiwa katika uzinduzi wa rasimu hiyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad (kulia), akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhan (katikati) na Mjumbe wa tume hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba (kushoto), akimkabidhi rasimu ya Katiba Mpya, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, ili kuizindua rasmi katika hafla iliyofanyika viwanja Karimjee Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiinyanyua juu rasimu ya Katiba mpya, wakati alipokuwa akiizindua katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (wa tatu kushoto) na Makamu wake, Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhan.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi rasimu hiyo, Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), akimkabidhi rasimu hiyo, Naibu Katibu Mkuu msataafu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha Rose Migiro, kwenye hafla hiyo. Anayeshuhudia katikati ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi rasimu hiyo, Kamu Mwekyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Theophil Makunga kwa niaba ya waandishi wa habari nchini.
Na Neema Mgonja, Dar es Salaam
RASIMU ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetolewa rasmi, jijini Dar es Salaam leo, huku ikipendekeza uwepo wa mgombe binafsi, pamoja na muundo wa Serikali tatu zitakazojumisha Serikali ya Tanzania Bara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Serikali ya Shirikisho.
Pia rasimu hiyo, imefutilia mbali uwapo wa nafasi za Ubunge wa viti maalumu, huku ikipendekeza ukomo wa ubunge wa kuchaguliwa kuwa wa vipindi vitatu pamoja na kutoa mamlaka kwa wananchi kuwawajibisha wabunge watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Rasimu hiyo, uliofanyika nje ya ukumbi wa Karimjee jijini, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, alisema rasimu hiyo, itakuwa na ibara 240, tofauti na ya itumikayo sasa ambayo ina ibara 152.
Jaji Warioba alisema kuhusiana na mgombea binafsi tume iliyozunguka nchi nzima, ilibahini kuwapo kwa maombi mengi ya kutaka kuwapo kwa nafasi ya mgombea binafsi atakayekuwa huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia kata hadi urais.
Alisema tume ilipendekeza hayo kwa kuzingatia haki za binadamu, pamoja na haki ya kuchagua na kuchaguliwa na kwamba uwepo wa vyama ulikuwa ukiwabana wengine wasio katika muunganiko wa vyama, kupata haki hiyo ya kuchaguliwa.
Aidha rasimu hiyo ya Katiba imetambua umri wa kugombe urais kuwa kuanzia miaka 40, huku rasimu hiyo ikitoa mamlaka ya matokeo ya urais kupingwa Mahakamani na waliokuwa wagombea katika kinyanganyiro husika.
Katika hilo pia, rasimu hiyo imeahinisha kwamba mgombea urais atakuwa mshindi mara tu atakapokuwa ameshinda kwa kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote za urais zitakazokuwa zimepigwa na kwamba rais mshindi atahapishwa baada ya siku 30 baada ya kushinda.
Kwa upande wa madaraka ya Rais, Rasimu hiyo imepunguza madaraka hayo kwa Rais, ambapo imependekeza Rais kufanya uteuzi wa Mawaziri na manaibu wake na kisha kuwasilishwa kwa Bunge kwaajili ya kupigiwa kura na uthibitisho.
Pia Bunge limepewa mamlaka ya kuthibitisha uteuzi wa Jaji Mkuu na Naibu wake, pindi atakapokuwa ameteuliwa na Rais kwa kufuata ushauri wa Tume ya utumishi wa Mahakama.
Jaji Warioba alisema katika suala la uundwaji wa Serikali, tume hiyo ilipata wakati mgumu kufikia maamuzi hasa kutokana na eneo hilo kukumbwa na maoni mengi yanayokidhana kutoka pande mbili za muungano.
Alisema baada ya tafakuri ya kina, tume iliona na kupitisha uwepo wa Serikali tatu, pamoja na kupunguza mambo ya muungano kutoka 22 hadi kufikia saba.
Kutokana na utaratibu huo mpya, rasimu hiyo inatambua Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uraia na uhamiaji, Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje.
Mambo mengine ya muungano ambayo yanatambuliwa na rasimu hiyo ni pamoja na Mambo ya Nje, Usajili wa Vyama vya Siasa pamoja na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
Rasimu ya Katiba mpya, pia imepunguza ukubwa wa uongozi wa Serikali kwa kupendekeza uwepo wa mawaziri wasiozidi 15, ambao pia hawatokuwa wabunge na ambao katiba itawabana kuhudhuria vikao vya Bunge hisipokuwa katika kipindi ambacho watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.
Jaji Warioba alisema rasimu hiyo imependekeza kuwapo na wabunge wa aina mbili wabunge wakuchaguliwa ambapo wabunge watakua 75 wabunge 20 kati yao wakitokea upande wa Zanzibar, 50 kutoka Bara na watano wa kundi la ulemavu ambao watateuliwa na Rais.
Alifafanua kuwa katika mgawanyiko huo, kutakuwapoa na majimbo 25 tu ya uchaguzi kwa Tanzania Bara ambao kila jimbo litatoa wabunge wawili huku ikizingatiwa nafasi moja ya uwakilishi wa mwanamke.
Pia rasimu hiyo imependekeza kufutwa kwa uchaguzi mdogo, na kwamba itokeapo nafasi ya ubunge imeachwa wazi na mbunge wa chama cha siasa, basi chama husika kiteue mtu wa kujaza nafasi hiyo.
Katika hilo pia rasimu hiyo imependekeza pia kuendelea kumtambua Mbunge ambaye atafukuzwa na chama chake cha siasa, hisipokuwa pale atakapohama chama ndipo ukomo wake wa ubunge utakapokuwa.
Rasimu hiyo imeweka wazi na kupendekeza Spika wabunge na Naibu wake kutotokana na wabunge ama wasiwe viongozi wa vyama vya siasa.
Kuhusiana na Tume huru ya Uchaguzi, tume hiyo kupitia Rasimu yake imependekeza kuunganishwa kwa Tume ya uchaguzi, kura ya maoni na Usajili wa Vyama vya Siasa.
Majina ya waombaji wa kushika nafasi hiyo, yanapaswa kuombwa na kupitiwa na kamati maalumu itakayokuwa ikiongozwa na Jaji Mkuu pamoja na Spika wa Bunge.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, Rasimu hiyo imeacha hoja ya Mahakama ya Kadhi kwa maelezo kuwa si la muungano na kwamba linaweza kuamuliwa na Serikali husika.
Rasimu hiyo ambayo jana ilizinduliwa na Makamu wa Rais Mohamed Ghalib Bilali, itasomwa na kabla kujadiliwa na wananchi kupititia mabaraza ya katiba yaliyoundwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment