TANGAZO


Friday, June 7, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Bilal afungua kongamano la ushindani wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akiteta jambo na aliyekua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, jijini Arusha leo. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wajumbe wa kongamano kuhusu ushindani kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World  Economic Forum), wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua Kongamano hilo, leo katika Hoteli ya New Arusha Hotel, jijini Arusha leo Juni 7/2013. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifungua kongamano kuhusu ushindani kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel, jijini Arusha             leo Juni 7/2013. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo (kushoto) na aliyekua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano kuhusu ushindani kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World  Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel, jijini Arusha leo Juni 7/2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World  Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel jijini Arusha leo Juni 7/2013. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki Richard Sezibera baada ya kufungua kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani( World  Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel jijini Arusha leo Juni 7/2013. 

No comments:

Post a Comment