Mawakili wanaowatete washtakiwa, viongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Farid Ahmed na wenzake, Salim Taufiq Ali (kushoto), Rajab Abdalla Rajab (katikati) na Abdalla Juma Mohamed, wakijadili jambo, nje ya Mahakama ya Rufaani Tanzania jana, baada ya kusikilizwa kwa rufani ya wateja wao, kupinga rufaa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa kuwa katika shauri lao hakuna hukumu yoyote iliyokwisha kutolewa na Mahakama Kuu ya Zanzibar. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mawakili wanaowatete washitakiwa, viongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Farid Ahmed na wenzake, wakiondoka Mahakama ya Rufaa baada ya kusikilizwa na mahakama hiyo jana. |
Askari Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi kwenye Mahakama ya Rufaa, wakati mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya Uamusho, walipokuwa kwenye chumba cha Mahakama kupeleka shauri lakupinga rufaa iliyofunguliwa na DPP, katika kesi ya viongozi hao, jijini Dar es Salaam jana.
|
Na Grace Gurisha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo inatarajia kutoa uwamuzi mdogo katika kesi ya kula njama inayomkabilia Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, baada ya mahakama kupitia hoja na sheria zilizowasilishwa na pande zote mbili.
Hoja ya upande wa utetezi ulidai kuwa Lwakatare kisheria dhamana ni haki ya msingi ya kwa kuzingatia washtakiwa wapo ndani kwa muda muda mrefu, ambapo upande wa Jamhuri ulidai kuwa huu si muda mwafaka wa utetezi kuomba dhamana.
Wakili wa utetezi Peter Kibatala alidai jana, mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana wa mahakama hiyo alidai shauri limekuja kwa kusikilizwa, ambapo aliomba mahakama itoe uwamuzi wa dhamana leo.
"Hoja zilizotolewa hakimu mwingine hawezi kutoa tarehe ya uwamuzi, kwa hiyo kwa sababu wewe hukuwepo na hoja zipo kwa maandishi, tunaomba mahakama yako itoe dhamana", alidai Kibatala.
Baada ya Kibatala kudai hivyo, hakimu Katemana alihoji juu ya kusikilizwa kwa shauri hilo, ambapo alisema katika kumbukumbu za mahakama zinaonesha kesi imekuja kwa kutajwa na si kusikilizwa.
Hata hivyo wakili wa Serikali Ponzino Lukos alidai kuwa katika kumbukumbu inaonesha kuwa shauri limekuja kwa kutajwa, Mei 13 mwaka huu mbele ya hakimu Sundi Fimbo upande wa utetezi walileta maombi ya dhamana.
Alidai maombi hayo yalijadiliwa mahakamani na Fimbo alidai kuwa hawezi kutoa uwamuzi, kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hiyo hayupo kwa hiyo iliahirishwa hadi Mei 27 mwaka huu kwa kutajwa, ambapo pia iliahirishwa hadi Juni 10 mwaka huu kwa kutajwa.
Mbali na Lwakatare mshtakiwa mwingine ni Ludovick Joseph ambapo wote wanakabiliwa na shtaka la kula njama la kumdhuru kwa sumu Denis Msacky, ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la Mwananchi.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa walikula njama , wakiwa Kimara Kingíongío Stopover,walitaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Msacky.
Awali wakili wa Lwakatare, Peter Kibatala alidai wanaamini katika faili kuna nakala ya uwamuzi uliyotolewa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam la ombi namba 14/2013.
Nakala hiyo niya uwamuzi uliyotolewa na Jaji Lawrence Kaduri wa kutupilia mbali mashtaka ya tuhuma za Ugaidi na kubaki na shtaka mmoja la kuala njama,ambalo lipo chini ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Hata hivyo alidai kuwa shtaka hilo linadhamana, inagawa hakimu anayesikiliza kesi hiyo,Katemana hayupo, lakini bado anaamini mahakama inaweza kutoa dhamana.
"Dhamana ni haki ya msingi ya mshtakiwa ukizingatia washtakiwa wapo ndani kwa muda muda mrefu na pia Lwakatare afya yake siyo nzuri,hivyo wanaiomba mahakama itoe masharti ya dhamana",alidai Kibatala.
Wakili wa Serikali Prudence Rweyongeza alidai kuwa huu si muda mwafaka wakuwasilisha maombi yao kwa kuwa uwamuzi wa Mahakama Kuu unaanza kufanya kazi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)kuwasilisha taarifa.
Machi 18 mwaka huu,Lwakatare na Joseph walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka manne yakiwemo ya Ugaidi,ambayo ilikuwa ni kesi namba 37 ya mwaka 2013.
Machi 20,2013,DPP aliwafutia mashtaka,lakini muda mfupi baadaye walikamatwa na kufunguliwa mashtaka hayohayo katika kesi namba 6 ya 2013.
Mawakili wanaomtetea Lwakatare hawakukubaliana na uamuzi huo,hivyo waliwasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakiupinga. Pia waliiomba mahakama hiyo itengue uamuzi huo.
Mwakaili hao ni Mabere Marando, Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, Lissu, Nyoronyo Kichere.
Wakili wa Serikali Mkuu,Rweyongeza akisaidiana na wenzake Peter Maugo na Ponsiano Lukosi alisema DPP alifuta mashtaka ya Lwakatare na mwenzake kwani kesi ya awali ilifunguliwa katika masjala isiyostahili.
Rweyongeza alidai kuwa kesi ya kwanza ilisajiliwa katika kitabu cha kesi zinazosikilizwa na Mahakama za chini,badala ya kitabu cha kesi zinazosikilizwa na Mahakama Kuu.
Pia alitaja sababu zingine kuwa, mahakama ilikosea kwa kuwaruhusu washtakiwa kujibu mashtaka ambayo husikilizwa na Mahakama Kuu pekee.
Katika sababu hizo Jaji Kaduri alisema Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP),hakukosea kufuta kesi namba 37 ya mwaka huu na kufungua kesi nyingine.
Lakini alikubaliana na hoja ya wakili wa Lwakatare, Tundu Lissu kuwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Lwakatare yalikuwa hayana uhalisia wa mashtaka ya Ugaidi.
No comments:
Post a Comment