TANGAZO


Thursday, June 13, 2013

Benki ya Diamond Trust yazindua huduma mpya ya DTB Touch 24/7

Mmoja wa wafanyabiashara akijiorodhesha kungia katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya kutoa na kuweka fedha kwa njia ya simu za mkononi ya DTB Touch 24/7, usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk wa bayana.blogspot.com)
Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, kuhusu huduma mpya ya kutoa pesa kwenye ATM za benki hiyo kwa njia ya simu za mkononi, iitwayo DTB Touch 24/7, ambapo mteja mwenye akauti kwenye mitandao yote ya simu, anaweza kutoa pesa kwenye ATM hizo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mikopo na Utawala, Joseph Mabusi, Mwenyekiti wa DTB, Abdul Samji, Mkurugenzi, Nasim Devji na Ofisa Mtendaji Mkuu, Viju Cherian.
Baadhi ya wafanyakazi wa DTB pamoja na wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa huduma hiyo, Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. 
Baadhi ya wafanyakazi wa DTB na wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa huduma hiyo, Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. 
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika uzinduzi huo, hotelini hapo, wakifuatilia habari zilizokuwa zikitolewa na uongozi wa benki hiyo.

Mwenyekiti wa DTB, Abdul Samji, akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa Mikopo na Utawala, Joseph Mabusi na kulia ni Mkurugenzi wa DTB, Nasim Devji.
Mwenyekiti wa DTB, Abdul Samji, Abdul Samji, akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati na katikati ni Mkuu wa Mikopo na Utawala, Joseph Mabusi. 
Baadhi ya wafanyakazi wa DTB na wageni mbalimbali wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika uzinduzi wa huduma hiyo, Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.


Mwenyekiti wa DTB, Abdul Samji, Abdul Samji, akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati, Mkuu wa Mikopo na Utawala, Joseph Mabusi Mkurugenzi wa DTB, Nasim Devji na Ofisa Mtendaji Mkuu, Viju Cherian.

Na Hamisi Magendela 

BENKI ya Diamond Trust (DTB), usiku wa kuamkia leo, imezindua huduma mpya, inayoitwa DTB Touch 24/7, ambayo inamuezesha mteja kutumia simu ya mkononi kupata huduma za kibenki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa kuzindua huduma hiyo, 
Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati, alisema kuwa huduma hiyo inapatikana kwa wateja wote, wanaotumia mitandao ya Tigo, Vodacom na mingineyo, inayopatikana nchini.

"Huduma hii inamsaidia mteja kutopata usumbufu wa kwenda katika tawi la benki hiyo, ili kupata huduma ya kifedha ikiwemo kuweka au kuchukua hali ambayo, itasaidia kupunguza msongamano usiokuwa wa lazima katika matawi ya benki hiyo yaliyopo nchini kote," alisema Bahati.


Aliongeza kuwa wateja wanaotumia mitandao hiyo ya simu watakuwa na uwezo wa kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao za mkononi, pia kutoa pesa kwenye ATM kupitia M Pesa, Tigo Pesa na nyinginezo kwa ushirikiano wa karibu na mawakala wa kampuni hizo za simu kwa mitandao yote.


Aliongeza kuwa huduma hiyo, imefanyiwa tafiti kwa kipindi kirefu na watafiti kuandika ripoti kadhaa hali inayofanya mfumo huo kuwa bora na usiokuwa na shaka kwa watumiaji kwa maana anaweza kupata huduma ya muda wa maongezi, kuchukua au kutoa fedha kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment