TANGAZO


Monday, May 27, 2013

Zantel yazindua Epiq Open Mic



Wasanii Diamond na Ney wa Mitego, wakiimba katika uzinduzi wa Epic Open Mic, Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na mpigapicha wetu)
 Msanii Godzila akiimba kwenye jukwaa hilo, viwanjani hapo jana. 
Msanii Mabeste akitumbuiza katika uzinduzi huo.
Msanii Madee, akitumbuiza kwenye uzinduzi huo, Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam.
Msanii Marco Chali, akielezea zoezi zima la Epiq Open Mic, litakavyoendeshwa kwenye Viwanja hivyo.
Wasanii Rama Dee na Mapacha wakiwa jukwaani, wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo.

Msanii Walter akiimba moja ya nyimbo zake kwenye uzinduzi huo.


KATIKA kuelekea msimu wa sita wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua Epiq Open Mic ikiwa ni nafasi nyingine kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha vipaji vyao kabla usaili wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.


Epiq Open Mic inatarajiwa kuwapa nafasi vijana kujifunza misingi ya muziki kutoka kwa mmoja wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini, Marco Chali.

Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.

Tamasha hilo la Epiq Open Mic, ambalo ni la bure litazinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke tarehe 26 ya mwezi huu ikisindikizwa na wakali kibao wa Bongo flavor kama Diamond Platnumz, Madee, Godzila, Ney wa Mitego, Mabeste na Mrap.

Akizungumza wakati wa kuzindua matamasha hayo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.

‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.

Baada ya uzinduzi wa tamasha la Epiq Open Mic Mwembe Yanga tamasha hilo litaendelea kila jumamosi kwenye makao makuu ya Zantel likiwapa nafasi vijana kujisajili na kurekod sauti zao.

Vijana watakaorekodi sauti zao watapigiwa simu na timu ya watayarishaji wa muziki chini ya Marco Chali pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri wa namna ya kuboresha muziki wao zaidi.

‘Zantel imejipanga kutumia fursa hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan.

Epiq Open Mic pia inatarajia kuwapa fursa ya kurekodi baadhi ya vijana watakaokua na vipaji.

No comments:

Post a Comment