TANGAZO


Friday, May 10, 2013

Wauguzi nchini kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani UDSM

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Mkoa wa Dar es Salaam, Joary Bigirwa (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, itakayoadhimishwa kimkoa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) keshokutwa. Shughuli za maadhimisho hayo zitaanza kesho viwanja vya UDSM, kwa kutoa huduma za vipimo vya maradhi mbalimbali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Tawi la Vyuo Vikuu Dar es Salaam, Wilhemina Niwabigira na kulia Ofisa Muuguzi UDSM, Agnes Innocent.

Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Tawi la Vyuo Vikuu Dar es Salaam, Wilhemina Niwabigira, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam, wakati walipozungumza nao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, itakayoadhimishwa keshokutwa Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo Shughuli za maadhimisho hayo, zitaanza kesho viwanjani hapo. Kushoto ni baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kwenye mkutano huo leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Tawi la Vyuo Vikuu Dar es Salaam, Wilhemina Niwabigira (DUCE), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati walipozungumza nao, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, itakayoadhimishwa keshokutwa Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo Shughuli za maadhimisho hayo, zitaanza kesho viwanjani hapo. Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Mkoa wa Dar es Salaam, Joary Bigirwa na kushoto ni Ofisa Muuguzi UDSM, Agnes Innocent.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Mkoa wa Dar es Salaam, Joary Bigirwa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Tawi la Vyuo Vikuu Dar es Salaam, Wilhemina Niwabigira na kulia Ofisa Muuguzi UDSM, Agnes Innocent.


Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Tawi la Vyuo Vikuu Dar es Salaam, Wilhemina Niwabigira (DUCE), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati walipozungumza nao, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, inayoadhimishwa keshokutwa Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Mkoa wa Dar es Salaam, Joary Bigirwa na kushoto ni Ofisa Muuguzi UDSM, Agnes Innocent.


Na Frank Shija – MAELEZO

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya wauguzi dunia itakayofanyika kimkoa katika viwanjwa vya chuo kikuu cha Dar es Salaam, kuanzia siku ya Jumamosi tarehe 11 na kufikia kilele tarehe 12 mei 2013.

Wito huo umetolewa  na mwakilishi wa chama cha wauguzi tawi la mkoa wa Dar es Salaam Bi. Joan Bigirwa  alipokuwa akiongea na waandishi wahabari leo, jijini Dar es Salaam.

Joan alisema kuwa kutokana na kaulimbiu ya mwaka huu kuhusu malengo ya millennia yanahusu vijana wameamua kufanyia maadhimisho hayo katika viwanjwa vya chuo kikuu ili kutoa fursa kwa vijana wengi kushiriki katika maadhimisho hayo.

Aidha amesema kwamba maadhimisho hayo yanataraji kuanza saa tatu asubuhu kwa maandamano kututoka Ubungo hadi viwanja vya Chuo Kikuu cha  na kupokelewa na mgeni rasmi ambaye atakuwa ni Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam.

Naye Mwenyekiti wa TANNA tawi la vyuo vikuu Bi. Wilhelmina R. Niwabigira ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataambatana na utoaji wa huduma mbalimbali.

Niwabigira ametaja baadhi ya huduma hizo zitakazotolewa ni ushauri nasaha,kupima saratani ya shingo ya kizazi na matiti,kupima kisukari,afya ya akili, presha na ushauri wa vicoba ambapo huduma zote zitatolewa bure.

Siku ya wauguzi dunia usherehekewa kila mwaka kwa kumkumbaka mwanzilishi wa uuguzi nchini Bi. Florence Nightngale.

No comments:

Post a Comment