Kiongozi maarufu wa kimila katika eneo la Abyei ameuawa kwa kupigwa risasi katika tukio lililohusisha wapiganaji wa kiarabu.
Kiongozi huyo Kual Deng Majok ambaye ni kiongozi mkuu wa ukoo wa Dinka aliuawa katika mapambano kati ya Kundi la Wapiganaji wa kiarabu la Misseriya na walinzi wa amani wa Umoja wa mataifa ambapo imeelezwa kuwa maafisa wa Kijeshi wa Umoja wa mataifa pia walijeruhiwa katika tukio hilo.
Jimbo la Abyei lenye utajiri wa mafuta linalogawanya lililo kati kati ya Sudan na Sudan kusini lilijitenga mwaka 2011,ambapo umiliki wake unagombewa na nchi zote mbili.
Chanzo cha mgogoro huo ni ugomvi wa ardhi kati ya Wakulima wanaoungwa mkono na serikali ya Sudan kusini wa kabila la Dinka Ngok na wafugaji wa Misserya wanaotoke upande wa kaskazini.
Kutokana na mgogoro Jimbo la Abyei limeendelea kuwa chiniya usimamizi wa Umoja wa vikosi vya umoja wa mataifa.
Tukio hilo la Jumamosi lilianza wakati vikosi vya jeshi la umoja wa mataifa lilipojaribu kuwaokoa maofisa wa kijeshi wa Sudan kusini wanaofuatilia hali ya baadae ya Jimbo la Abyei,baada ya kuzingirwa na wapiganaji wa Misseriya.
Msemaji wa Kundi la Dinka aliwaambia waandishi wa habari kuwa Kiongozi wao mkuu Kual Deng Majok aliuawa baada ya kushambuliwa na wapiganaji wa Kundi la Misseriya,ambapo tukio hilo pia limethibitishwa na mkuu wa kundi la Misseriya,ambaye kwa upande wake amesema wapoganaji wa Kundi la Misseriya walisimamisha msafara wa maafisa wa sudan kusini na kuanza majadiliano ambapo askari mmoja katika jeshi la Umoja wa mataifa alimpiga risasi mpiganaji mmoja wa kundi hili aliyekuwa akijiandaa kutoa silaha yake.
Sudan na Sudan kusini zimekuwa katika kipindi kirefu migogoro ya kidini na kikabila kilichosababisha vita ya kikabila ambavyo vimegharimu maisha ya watu zaidi milioni moja na nusu
abyei_arab_wapiganaji
No comments:
Post a Comment