TANGAZO


Friday, May 17, 2013

Wananchi wengi wajitokeza Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, mjini Dodoma

Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Bima ya Afya, Grace Michael akimpa maelekezo juu ya shughuli za mfuko Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA, Jayne Nyimbo.
Mmoja kati ya watu walihudhuria maonesho hayo akipatiwa huduma ya afya na afisa wa NHIF.
Ofisa Masoko wa SSRA, Naima Bakari akitoa maelezo ya kazi Kuu za Mamlaka kwa wananchi wa Dodoma.
Mmoja kati ya wananchi wa Dodoma akijiandikisha katika banda la SSRA.
Ofisa Masoko wa SSRA, Naima Bakaria kitoa maelezo ya kazi kuu za Mamlaka kwa wananchi wa Dodoma.
Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Arden Rage akijiandikisha katika banda la GEPF baada ya kupata maelezo ya Mfuko kutoka  kwa Aloyce Ntukamazina na Josephat Mshana.
 Lewis Ngirwa (kulia), akielezea faida ya kujiunga na Mfuko wa GEPF.
Ofisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akimkabidhi kitambulisho cha uanachama Mbunge wa Viti Maalum, Margaret Agnes Mkanga,  mara baada ya kujiunga na PPF alipotembelea banda la mfuko huo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoani Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa PPF, kutoka kulia ni Ofisa Majanga wa Mfuko, Noel Assenga, Meneja  Uhusiano, Lulu Mengele na Mhasibu wa PPF, Grace Fihavango, alipotembelea banda PPF.

No comments:

Post a Comment