Serikali kuzindua uhamasishaji matumizi ya lishe bora nchini
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kuhusu hali ya lishe nchini, mkakati wa Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata virutubisho muhimu kupitia vyakula na kampeni ya uhamasishaji wa matumizi ya Lishe Bora nchini, itakayozinduliwa tarehe 16, mwezi huu na Rais Jakaya Kikwete, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, ikiongozwa na kauli mbiu "Lishe bora ni Msingi wa Maendeleo, Timiza wajibu wako". (Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO)
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Faith Magambo, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu madhara yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora kwa watoto na umuhimu wa maziwa ya mama katika kujenga afya bora ya mtoto. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo akipokea na kujibu maswali ya waandishi wa habari, wakati alipozungumza nao katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo leo, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment