Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipata
maelezo wakati alipotembelea sehemu za Kihistoria zilizopo katika mji wa
Beijing nchini China kiwa katika ziara ya Kiserikali na ujumbe wake. (Picha na
Ramadhan Othman, China)
Mke wa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwamamwema Shein, akiangalia kitabu
wakati alipotembelea makumbusho ya kihistoria katika Mji wa Beijing nchini China, katika ziara ya Kiserikali
kwa mwaliko wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Kulia ni Balozi Mdogo wa
China anayefanyia kazi zake Zanzibar, Bibi Chen Qiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na ujumbe wake
wakitembelea sehemu mbalimbali za
Kihistoria zilizopo katika Makumbusho ya Mji wa Beijing, nchini China akiwa katika ziara
ya Kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na mkewe, Mama Mwamamwema
Shein katika Viwanja vya Makumbusho ya Kihistoria nchini China pamoja
na ujumbe waliofuatana nao katika
ziara ya Kiserikali.
Pichani linaonekana moja wapo ya Majengo yaliyokuwemo
katika eneo kubwa la kumbukumbu za kihistoria katika mji wa Beijing, ambapo
wananchi wa China wamekuwa na ukarimu wa aina yake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kusoto), pamoja na ujumbe
aliofuatana nao, akiuliza swali kwa waongozaji na watoa maelezo katika sehemu za
kihistoria zenye kumbukumbu nyingi, zinazotembelewa na wageni mbalimbali katika mji huo, wa Beinjing nchini
China, akiwa katika ziara ya Kiserikali ya siku saba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiuliza suala kwa waongozaji na
watoa maelezo katika sehemu za kihistoria zenye kumbukumbu nyingi, zinazopelekea
wageni wa aina tofauti kutembelea katika mji huo wa Beinjing nchini China.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na Naibu Waziri wa Biashara wa
China Liu Cigui, wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa World Hotel China, ambapo walifanya
mazungumzo na kutiliana saini makubaliano ya masuala ya Biashara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Fedha na Uchumi wa Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, akitiliana saini makubaliano ya
kibishara kwa upande wa Serikali ya Zanzibar na Naibu Waziri wa Biashara wa
China, Liu Cigui katika ukumbi wa mikutano wa China World Hotel, huku wakishudiwa na
baadhi ya Mawaziri na Maofisa wa Serikali zote mbili, za Zanzibar na China.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Fedha na Uchumi wa Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, akibadilishana hati walizosaini mkataba ya uhusiano wa Biashara na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Liu
Cigui, katika ukumbi wa mikutano wa China World Hotel.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipeana mkono wa shukurani na Naibu Waziri wa Biashara wa China
Liu Cigui, baada ya kutiliana saini makubaliano katika nyanja za kibiashara kati
ya Serikali ya China na Zanzibar, ukumbi wa mikutano wa World Hotel China.
No comments:
Post a Comment