TANGAZO


Wednesday, May 15, 2013

Rais Kikwete atembelea Viwanda vya BIDCO Oil na AZAM jijini Dar es Salaam


Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na wadau wa lishe bora kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa  wakizindua mpango wa kuweka virutubisho vya lishe bora katika bidhaa za unga na mafuta 

nchini uliofanyika katika kiwanda cha BIDCO Oil and Soa kilichopo 

katika eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. (Picha 

zote na Freddy Maro)

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mafuta yaliyowekwa virutubisho vya lishe 

bora wakati alipokitembelea kiwanda cha BIDC Oil and Soap kilichopo eneo la viwanda 

la Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete akiangalia moja ya aina ya mafuta ya kula yanayotengenezwa kiwandani hapo.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akongea na wafanyakazi wa 

kiwanda cha BIDCO Oil and Soap muda mfupi baada ya kuzindua 

mpango wa kuweka virutubisho bora vya lishe katika bidhaa za unga 

na mafuta uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.


Mtaalamu wa kusaga unga Bwana Patrick Muriuki(kulia) 

akimwongoza Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuweka virutubisho 

vya lishe bora katika unga kwa kutumia teknolojia ya kisasa wakati 

Rais alipotembelea Kiwanda cha   Azam kinachomilikiwa na S.S. 

Bhakressa Buguruni jijini Dar esSalaam kukagua uwekaji wa 

virutubisho vya bora katika bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo.



Rais Dk. Jakaya kikwete akiangalia ukaguzi wa uwepo wa 

virutubisho vya lishe bora katika bidhaa zinazozalishwa katika 

kiwanda cha kuzalisha unga AZAM ukifanyika katika maabara ya 

kiwanda  hicho Buruguruni jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment