Guard Maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja (hayupo pichani), ikitoa heshima kabla ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini lililofanyika leo, Mei 28, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro. Picha na Felix Mwagara.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kulia), akimvalisha Nishani ya Utumishi Uliotukuka kazini, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamis Nkubasi. Jumla ya Maafisa na Askari 30 kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamevalishwa Nishani mbalimbali leo, Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa Nishani mara baada ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini leo, Mei 28, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment