TANGAZO


Wednesday, May 29, 2013

CUF kukutana na wananchi wa Mtwara jijini Dar es Salaam Juni 2

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Julius Mtatiro, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho, kukutana na wananchi wa Mtwara, jijini Dar es Salaam Juni 2. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Salim Mandari. 


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Julius Mtatiro, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho, kukutana na wananchi wa Mtwara, jijini Dar es Salaam Juni 2. Kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, Mbarallah Maharagande.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Julius Mtatiro, akifafanua jambo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho, kukutana na wananchi wa Mtwara, jijini Dar es Salaam Juni 2, mwaka huu, Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni. Kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, Mbarallah Maharagande.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Julius Mtatiro, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho, kukutana na wananchi wa Mtwara, jijini Dar 
es Salaam Juni 2, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Salim Mandari na kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, Mbarallah Maharagande.


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Julius Mtatiro, akielezea jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya  waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho, kukutana na wananchi wa Mtwara, jijini Dar es Salaam Juni 2, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Salim Mandari.

Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, wakati alipokuwa akizungumza nao, jijini Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho, kukutana na wananchi wa Mtwara, jijini Dar es Salaam Juni 2, mwaka huu, Ofisi Kuu ya Chama hicho, Buguruni.



Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, akijibu maswali ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipozungumza nao kuhusu chama hicho, kukutana na wananchi wa Mtwara, jijini Dar es Salaam Juni 2, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Salim Mandari na kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, Mbarallah Maharagande.


Na Nyendo Mohamed
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeandaa mkutano utakaowakutanisha wenyeji wa mkoa wa Mtwara na Lindi waishio jijini Dar es Salaam, ili kujadili suala la gesi asilia, iliyoko katika Mikoa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaofanyika Juni 9 mwaka huu, utahusisha pia baadhi ya wawakilishi kutoka katika mikoa hiyo.

Alisema mtoa mada katika mkutano huo, atakuwa mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye ataeleza mikakati ya kuwekwa hili gesi hiyo iweze kuwanufaisha watu wa mikoa hiyo na Taifa kwa ujumla.

Mtatiro alisema CUF imefikia hatua hiyo, kutokana na Serikali kuzuia wanasiasa kufanya mikutano katika Mkoa Mtwara na wananchi wa mkoa kutoa malalamiko wakitaka elimu juu ya rasilimali gesi .

Alisema maazimio ambayo wananchi watayatoa katika mkutano huo, yatawasilishwa kwa Serikalini ikiwa ni pamoja na kwa Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anne Makinda pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

Aliongeza kuwa Serikali haikujipanga toka awali kushughulikia vyema suala hilo, jambo lilosababisha kutokea kwa vurugu zilizotokea na kwamba inahitajika busara zaidi kutafuta ufumbuzi.

''Serikali haikufanya juhudi ya kutafuta wananchi na kuongea nao kuhusiana na swala hili la gesi na ni jambo ambali lilisababisha kutokea kwa vurugu hizo''

Pia alisisitiza kuwa Serikali inatakiwa kujipanga ni si kutumia nguvu katika swala hili kwani wananchi wanahaki ya kufahamu kuhusiana na rasilimali zao na kuwataka wananchi kujitokeza katika mkutano huo ili kujadili swala hilo la msingi ambalo linaweza kuchangia maendeleo katika nchi yetu.

No comments:

Post a Comment