TANGAZO


Monday, May 13, 2013

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Kituo cha Biashara na Uchumi cha UDSM (UDEC), vyawapa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiri wanafunzi waliomaliza chuo hicho hivi karibuni

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. Annacleti Kashuliza akifungua mafunzo ya wiki 3 ya Vijana 40 waliohitimu masomo ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, miaka ya hivi karibuni, ambao hawana kazi leo, jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo kwa vijana yanalenga katika kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi ya maendeleo na kuwafanya waweze kuajiri vijana wengine pamoja na kusaidiwa kupata fedha benki kwa ajili ya kuanzisha biashara kutokana na michanganuo watakayoiwasilisha. (Picha zote na Aron Msigwa, MAELEZO)


Sehemu ya Vijana 40, waliohitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), miaka ya hivi karibuni, ambao hawana ajira wakiwa katika mafunzo ya wiki 3 ya kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi itakayowajengea uwezo wa kuajiri vijana wengine, wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye mafunzo hayo chuoni hapo leo. Mafunzo hayo yanafanyika sehemu ya Biashara na yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), pamoja na Kituo cha  masuala ya Biashara na uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDEC), ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wa Vyuo Vikuu nchini. 


Baadhi ya Vijana 40, waliohitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), miaka ya hivi karibuni, ambao hawana ajira wakiwa katika mafunzo ya wiki 3 ya kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi itakayowajengea uwezo wa kuajiri vijana wengine. Mafunzo hayo yanayoendelea chuoni hapo, sehemu ya Biashara na yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), pamoja na Kituo cha  masuala ya Biashara na uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDEC), ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wa Vyuo Vikuu nchini. 

1 comment:

  1. Good wakafanyie kazi hayo mafunzo. Afu serekeli iwasaidie ili mafunzo yasibaki kama walivyokuja.

    ReplyDelete