Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari karibu na shule moja katika mji mkuu wa Syria Damascus, limelipuka.
Inaarifiwa kuwa kuna majeruhi kadhaa kutokana na mlipuko huo.
Mlipuko wenyewe ulitokea katika mtaa wa Mazzeh, Kusini Magharibi mwa mji mkuu na inaaminika kuwa lilikuwa shambulizo la kujitoa mhanga.
Shirika la habari la serikali limeripoti kuwa shambulio hilo lilikuwa la kigaidi.
Kituo cha televisheini kinachosimamiwa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la
Hezbollah , kilisema kuwa shambulio hilo lililenga kumuua waziri mkuu wa nchi hiyo ingawa aliponea.
Hezbollah , kilisema kuwa shambulio hilo lililenga kumuua waziri mkuu wa nchi hiyo ingawa aliponea.
Waziri mkuu huyo, Wael al-Halki aliponea shambulizi hilo kwani lilikuwa limelenga msafara wa magari yake mjini Damascus.
Picha iliyowekwa kwenye mtandao na kundi hilo, ilionyesha moshi mkubwa angani ukitoka katika eneo la shambulio.
Duru kutoka kwa shirika la kutetea haki za binadamu la Syria na ambalo lina makao yake nchini Uingereza lilisema kuwa mtu mmoja aliyekuwa na waziri mkuu wakati wa shambulio hilo aliuawa.
No comments:
Post a Comment