Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa (kushoto), akiwaonesha warembo wa Kitongoji cha Dar Indian Ocean, gazeti hili jinsi linavyotayarishwa, ikiwemo uwekwaji wa habari mbalimbali. Wa pili kushoto ni Mwandishi mwandamizi, Eben-ezeri Mende.
Mpigapicha Mkuu wa Gazeti hilo, Richard Mwaikenda akiwaelezea warembo hao, jinsi ya upatikanaji wa picha za habari na jinsi ya kuziandikia maelezo yake kabla ya kuwekwa gazetini jana.
Mhariri wa Michezo, Deo Myonga, akiwaonesha warembo hao, habari za michezo na burudani, jinsi zinavyoandikwa na kupangwa kwenye kurasa za gazeti, walipotembelea Ofisi za gazeti la chumba cha habari jijini leo.
Msanifu kurasa wa Jambo Leo, Chris Shola, akiwaonesha warembo hao, jinsi gazeti hilo, linavyosanifiwa.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayomiliki magazeti ya Jambo Leo, Staa Spot, Dar Metro na jarida la Jambo Brand, Beny Kisaka (kulia), akizungumza jambo na warembo hao, walipomtembelea ofisini kwake leo.
Warembo wa Kitongoji cha Dar Indian Ocean, wakiwa katika picha mara baada ya kumaliza ziara yao, Ofisi za Gazeti la Jambo Leo, Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment