Pages

Thursday, April 18, 2013

Ujumbe wa FIFA watembelea Ofisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jijini Dar es Salaam



Ofisa Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi, akisistiza jambo, Dar es Salaam leo, alipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. (Picha zote na Idara ya Habari, Maelezo)


Mkurugenzi wa Maendeleo ya  Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Loenard Thadeo (kushot), Mkurugenzi wa Habari, Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Msaidizi wa Michezo Juliana Yasoda na Ofisa Habari Mkuu wa Wizara, Godlease Malisa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Seth Kamuhanda hayupo kwenye picha, wakati ugeni kutoka Shirikisho la Mpira duniani (FIFA), walipotembelea Ofisi za Wizara leo jioni.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Seth Kamuhanda (wa kwanza kulia), akimsikiliza mwakilishi wa FIFA (wa kwanza kushoto), aliyekuja nchini kutatua mgogoro uliokuwepo kwenye uchaguzi wa Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu nchini. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodgar Tenga, ukumbi wa Wizara ya Habari leo, jijini Dar es salaam.


Wawakilishi wa FIFA, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda (aliyekaa). Katikati ni baadhi ya viongozi wa Wizara na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzaznia (TFF), wakiongozwa na Rais wake, Leodgar Tenga  (aliyeketi wa kwanza kushoto.

No comments:

Post a Comment