TANGAZO


Tuesday, April 23, 2013

Shaaban Mhamila 'Star Boy' ajifua kumkabili Jibaba Mei Mosi jijini Dar es Salaam

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini, Habibu Kinyogoli (kushoto), akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Shabani Mhamila 'Star Boy',  katika kambi ya Ilala iliyopo, Amana CCM leo. 'Star Boy' anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika siku ya Mei Mosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Super D, Mnyamwezi)


Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' (kushoto), akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe', mabondia wote wanajiandaa kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika siku ya Mei Mosi, ukumbi wa PTA Sabasaba.
Shabani Mhamila 'Star Boy', akionesha uwezo wa kugadi wakati alipokuwa akifanya mazoezi leo.
Ibrahimu Class 'King Class Mawe', akioneshana ujuzi wa kutupiana makonde na Shabani Mhamila 'Star Boy' kwenye mazoezi yao jijini leo.

Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' (kushoto), akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Chalo Issa, wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya ngumi ya Ilala. Star Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika Mei Mosi, Ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' (kushoto), akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe, wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya ngumi ya Ilala. Star Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika Mei Mosi, ukumbi wa PTA Sabasaba.

No comments:

Post a Comment