Katibu Tawala wa Mkoa, ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, akiongea neno kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Saidi Sadiki (kulia), kuzungumza kwa ajili ya kufungua kikao cha bodi hiyo, Dar es Salaam leo asubuhi jijini. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjISXXCLt3uifDQIg7fiUeIrprxS07bhN2_DRI1o96XbDvfX8dSS0EUP_Ecp4fZbLYSsSkCa3NMGMWcazn7Jg_444OUQ-N1dMJkBszZCwDswM0KdQpq0WcioRvH8-Z6TleHL4Pe7yVYWn1s/s640/IMG_2099.jpg)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Theresia Mmbando, wakinyamaza kimya kwa dakika moja kabla ya kukifungua kikao cha Bodi hiyo, kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea wananchi waliopoteza maisha na majeruhi wa jengo la ghorofa 16, lililoporomoka katikati ya jiji la Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita, ambapo jumla ya watu 34, walipoteza maisha.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa, wakinyamaza kimya kwa dakika moja kabla ya kufunguliwa kikao chao cha Bodi hiyo, kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea wananchi waliopoteza maisha na majeruhi wa jengo la ghorofa 16, lililoporomoka katikati ya jiji la Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita, ambapo jumla ya watu 34, walipoteza maisha.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3JE5VRbOaSu2qdyYmtkSujXP-BjhUic9fBfeTCKuadRi8vef0CI5RpEHDCDQNS0r8TmDmPlJ6uC336BvSxjBNrP50AhhihsLeAmOZq_y2hgmDMeH1GF6jBDXsasmdrG1Ez6Rbse3zs959/s640/IMG_2114.jpg)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa, Saidi Sadiki, akizungumza wakati alipokuwa akikifungua kikao cha bodi hiyo leo asubuhi jijini. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa, ambaye pia ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.
Wakuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) na wa Temeke, Sophia Mjema, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, alipokuwa akizungumza wakati akikifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa leo asubuhi.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, wakati alipokuwa akikifungua kikao cha Bodi hiyo jijini leo asubuhi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa, Saidi Sadiki, akizungumza wakati alipokuwa akikifungua kikao cha bodi hiyo leo asubuhi.
Wabunge wa Temeke, Abbas Mtevu (kushoto) na wa Viti Maalum, mkaoni Dar es Salaam, Mariam Kisangi, wakifungua makabrasha ya ripoti ya kikao kilichopita cha bodi hiyo, wakati wa kikao hicho, kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki jijini leo.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu (kulia), akifunua kabrasha pamoja na wajumbe wenzake wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kikao cha bodi hiyo leo asubuhi jijini.
Naibu Meya wa Temeke, Noel Kipangule, akizungumza wakati alipotakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki mara baada ya kukifungua kikao cha bodi hiyo, leo asubuhi jijini.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu, akizungumza katika kikao hicho cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kuhusu kuharibika kwa miundombinu ya kupitishia maji taka na mvua pia kuchimbika kwa barabara za jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtevu, akilalamika kuhusu kutokuzingatiwa ugavi sawa katika ujenzi wa barabara za jimbo lake huku majimbo mengine yakipata upendeleo wa dhahiri. Kulia ni Mbunge wa Viti maalum wa Dar es Salaam, Mariam Kisangi.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Eugen Mwaiposa, akilalamika kuhusu kutotendewa haki kwa ujenzi wa barabara za jimbo lake hilo.
Baadhi ya wageni waalikwa, wakisikiliza hoja na majadiliano mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wakati wa kikao chake hicho, kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki jijini leo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, wakifunua makabrasha ya kikao hicho, huku wakifuatilia hoja na majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kwenye kikao cha bodi yao, leo asubuhi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa, Saidi Sadiki, akizungumza wakati alipokuwa akikiongoza kikao cha hiyo jijini leo asubuhi. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa, Theresia Mmbando.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa pamoja na Ofisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Adrophina Ndyeiki (wa pili kulia), wakifuatilia na kuandika matukio ya mijadala pamoja na hoja zilizokuwa zikitolewa kwenye kikao hicho leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment