TANGAZO


Wednesday, April 3, 2013

Bozize adai Chad ilichangia kumpindua



Aliyekuwa rais wa CAR Francois Bozize
Rais aliyeng'olewa mamlakani katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ametuhumu serikali ya Chad kwa kuwasaidia waasi waliompindua mwezi jana.
Francois Bozize, aliambia BBC, kuwa wanajeshi maalum wa Chad waliongoza operesheni ya mwisho ya waasi mwezi jana pamoja na kuwaua wanajeshi wa Afrika Kusini.
Chad, ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa dharura wa kikanda kuhusu Afrika ya kati, haijajibu tuhuma hizo.
Bwana Bozize alisema kuwa aliomba kushirikishwa kwenye mkutano huo lakini akakataliwa.
Lakini rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ni mmoja wa marais wanaohudhuria mkutano huo wa nchi za Magharibi.
Wanajeshi kumi na watatu wa Afrika Kusini waliuawa kwenye makabiliano mjini Bangui, wakati waasi wa kundi la Seleka, walipotwaa mamlaka baada ya mkataba wa amani uliokuwa umependekezwa na rais Bozize kutupiliwa mbali.
Tukio hilo limesababisha taharuki nchini Afrika Kusini. Chama tawala ANC, kimekanusha madai kuwa wanajeshi walikuwepo nchini humo kwa sababu ya maslahi yake ya uchimbaji madini.
Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa wanajeshi wake walikuwa wanatoa mafunzo kwa majeshi ya serikali.
Wiki jana bwana Zuma, alisema kuwa wanajeshi wa Afrika Kusini, walifariki katika makabiliano makali yaliyochukua masaa tisa kupambana na waasi.
Bwana Bozize, alitwaa mamlaka katika mapinduzi mwaka 2003 na kushinda uchaguzi mara mbili anasema ameshangazwa na hatua ya Chad.

No comments:

Post a Comment