TANGAZO


Saturday, April 27, 2013

Asnath awa Redd's Miss Higher Learning Morogoro 2013

Washiriki wa shindano la  Redd’s Miss Higher Learning, Mkoa wa Morogoro wakicheza shoo ya ufunguzi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu (Higher Learning), mkoani humo. 

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Tarchisic Mtui, akipita mbele ya majaji na kivazi cha ubunifu alichokitengeneza kwa majani ya Mti wa Muashock  wakati wa shindano hilo, lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo. 

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange, akitembea kwa madaha mbele ya majaji na kivazi cha ufukweni wakati wa shindano hilo, lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo.

Mmoja wa washiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, akipita mbele ya majaji na kivazi cha ufukweni wakati wa shindano hilo, lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo.

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoani Morogoro, Hellen Mhando akipita jukwaani kujinadi mbele ya majaji na kivazi cha usiku wakati wa  Shindano hilo, lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo.

Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, wakiwa katika picha ya pamoja maara baada ya kutajwa wakati wa shindano hilo, lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo. Kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce, Hellen Mhando, Tausi Idd na Asnath Mwakitwange. 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, ‘Bongo Fleva’ Barnaba Boy akitumbuiza mashabiki wa tasnia ya urembo wakati wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakati wa wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo.
  
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao, kutawazwa kuwa washindi wa Shindano hilo, usiku wa kuamkia leo katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10, waliokuwa akiwania nao taji hilo


Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro, usiku wa kuamkia leo. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10, waliokuwa akiwania nao taji hilo. (Picha zote na Mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment