TANGAZO


Sunday, March 17, 2013

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Anjela Kairuki awa mgeni rasmi mbio za Ilala Nusu Marathoni, Mbunge Zungu ashiriki mbio hizo

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na washiriki wa mbio za Ilala Nusu Marathoni kabla ya kunzishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba (kushoto kwa Mbunge Zungu), Viwanja vya Garden Ilala Bungoni. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akizungumza na washiriki wa mbio hizo kabla ya kuzianzisha leo.


Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakifanya mazoezi kabla ya kuanza mbio hizo leo, Viwanja vya Garden, Ilala Bungoni. 




Mbunge Zungu akifanya mazoezi na washiriki wenzake wa mbio hizo kabla ya kuanzishwa na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, Viwanja vya Garden, Ilala Bungoni Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akiwa na filimbi tayari kuanzisha mbio hizo. Kulia kwake ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu ambaye naye alishiriki mbio hizo.


Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakipita kwenye mzunguko wa Barabara ya Uhuru na Msimbazi, Kariakoo kuelekea Mnara wa Saa, Mnazi Mmoja kabla ya kurudi tena kwenye Viwanja vya Garden, Ilala Bungoni kumalizia mbio hizo.


Mshiriki akipatiwa maji ya kunywa, kwenye kituo cha Kamata, makutano ya Barabara za Nyerere, Msimbazi, Nkurumah na Gerezani Railway, akielekea kwenye barabara ya Kawawa na kisha Lindi kuingia Bungoni kwenye viwanja vya Garden kwa ajili ya kumaliza mbio hizo.


Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakipita kwenye mzunguko wa Kamata kuelekea Barabara ya Kawawa na kisha mtaa wa Lindi kwenda Bungoni kwenye Viwanja vya Garden, kumalizia mbio hizo.


Washiriki wa mbio hizo, wakipita kwa kasi kwenye mzunguko wa Kamata kuelekea Barabara ya Kawawa na kisha mtaa wa Lindi kwenda Bungoni kwenye Viwanja vya Garden, kumalizia mbio hizo.


Mshiriki binafsi wa mbio za kujifurahisha katika mbio hizo za Ilala Nusu Marathoni, akiingia kwenye Viwanja vya Garden, Ilala Bungoni kumaliza mbio hizo.


Baadhi ya washiriki wa mwanzo, kuingia kwenye Viwanja vya kumalizia mbio hizo, wakiingia kwa kasi kwa ajili ya kugusa utepe wa kumalizia.


Mshindi wa kwanza wa mbio za Ilala Nusu Marathoni, akizungumza na kuhojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mbio hizo kwenye viwanja hivyo leo.


Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanawake, Lulu Gaitani, mara baada ya kumaliza mbio hizo.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akizungumza na jambo na mgeni rasmi katika mbio hizo, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Anjela Kairuki kwenye viwanja vya Garden, Ilala jijini Dar es Salaam leo.


Katibu wa Wazazi, Wilaya ya Ilala, Ruth Mutashaba, akimpatia zawadi ya fedha taslim mmoja wa washindi wa nafasi za kumi bora wa mbio hizo.


Katibu wa Wazazi, Wilaya ya Ilala, Ruth Mutashaba, akimpatia zawadi ya fedha taslim mmoja wa washindi kumi bora wa mbio hizo.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Ernest Chale, akimpatia zawadi ya fedha taslim mmoja wa washindi kumi kwa upande wa wanawake wa mbio hizo.


Ofisa Michezo, Mkoa wa Dar es Salaam, Adorph Halii, akimkabidhi zawadi ya fedha, mmoja wa vijana chini ya umri wa miaka 18, aliyeshiriki na kumaliza mbio hizo.


Ofisa Michezo, Mkoa wa Dar es Salaam, Adorph Halii, akiwakabidhi zawadi za fedha taslim, vijana chini ya umri wa miaka 18, walioshiriki na kumaliza mbio hizo.



Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu, akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za Ilala Nusu Marathoni kwa upande wa wanawake, Lulu Gaitani wakati wa kutunukiwa zawadi kwa washindi wa mbio hizo, Viwanja vya Garden, Ilala Bungoni, Dar es Salaam leo. Kushoto Ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba. 


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akimkabidhi zawadi ya fedha taslim, mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanawake, Lulu Gaitani, mara baada ya kuwavalisha nishani washindi wa nafasi tatu za mwanzo kwa upande wa wanawake.


Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Anjela Kairuki, akimvisha medali ya dhahabu, mshindi wa kwanza wa mbio za Ilala Nusu Marathoni, John Silima, wakati alipokuwa akiwatunuku zawadi washindi wa mbio hizo, Viwanja vya Garden, Ilala Bungoni, Dar es Salaam leo.



Mgeni rasmi wa mbio za Ilala Nusu Marathoni, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Anjela Kairuki, akizungumza na washiriki wa mbio za Ilala Nusu Marathoni, mara baada ya kuwatunuku zawadi washindi wa mbio hizo, Viwanja vya Garden, Ilala Bungoni, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment