TANGAZO


Thursday, March 28, 2013

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi azindua Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati), akiwa na muasisi wa mfuko wa Elimu wa Bonnah Trust Fund, Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, (kushoto), mara baada ya kuuzindua rasmi mfuko huo, Hoteli ya Hyatt, zamani Kilimanjaro kwenye hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo, Wakili wa kujitegemea, Mary Mnyiwasa.
Mwasisi wa mfuko huo, Bonnah Kaluwa akiwa katika pozi.
Mwasisi wa mfuko huo Bonnah Kaluwa (kulia), Mratibu wa matukio, Regina Ogwal 
(kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo, Mary Mnyiwasa, wakiwa mbele ya bango 
la mfuko huo.
Mwasisi wa Mfuko huo Bonnah Kaluwa, akitoa hutuba fupi kuhusu mfuko huo mbele ya wageni waalikwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
Mwasisi wa Mfuko huo Bonnah Kaluwa (katikati), akiwa na washauri wake wa masuala mbalimbali. Kushoto ni  Suzan Okayo na Regina Agwal.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe (katikati), akiwa na Mwasisi wa Mfuko huo Bonnah Kaluwa na mgeni mwalikwa ambaye jina lake alikufahamika mara moja.

 Mshauri wa masuala mbalimbali wa Mwasisi wa Mfuko huo Bonnah Kaluwa, Regina Agwal (katikati), akiwa na jamaa zake waliofika kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.

 Viongozi mbalimbali wa Kata ya Kipawa, wakiwa kwenye hafla hiyo, Hoteli ya Hyatt, usiku wa kuamkia leo.

 Diwani Bonnah Kaluwa akiwa na matoto wake aitwaye Vanesa (kulia). Kushoto ni rafiki wa mtoto wake huyo.

 Diwani Bonnah Kaluwa akiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilala, Situ Mwasa (kulia) na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ilala, Fatuma.

 Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.

 Mtoto wa Diwani Bonnah, Vanesa (kushoto), akiwa na rafiki yake kwenye hafla hiyo.

 Hawa nao walikuwepo katika uzinduzi huo.

 Diwani Bonnah Kaluwa akiwa amepozi na mmoja wa wageni waalikwa.     

 Diwani Bonnah Kaluwa akiwa na dada yake, Aziza Hassan.  

 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia), akiwa kwenye hafla hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Ilala. Kutoka 
kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, Mbunge wa Ukongo na  Eugen Mwaiposa (mwenye kilemba)

 Wasanii wa Kikundi cha Safi wakionesha sarakasi,katika hafla hiyo.

 Wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Msanii wa kikundi cha sanaa cha Safii, Abdulraufu Kawambwa, Mjukuu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akionesha umahiri wa kupitisha mfano wa surulia ambayo ipo wazi katika mwili wake kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mfuko huo.

 Mshauri wa Diwani Kaluwa Regina (kushoto), akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Eugen Mwaiposa kwenye hafla hiyo.

 Wasanii wa kikundi cha Safi wakiaga wageni waalikwa baada ya kumaliza kutoa burudani.

 Mwasisi wa Mfuko huo Bonnah Kaluwa (wa pili kulia), Diwani Kalua, akiwa na wageni waalikwa.

 Diwani Bonnah Kaluwa, akiserebuka kwa sebene na shemeji yake baada ya uzinduzi wa mfuko huo.

Mshauri wa masuala mbalimbali wa Diwani Bonnah Kaluwa, Suzan akiwa na mtoto wa diwani huyo baada ya uzinduzi huo.



Na Dotto Mwaibale


WATANZANIA wameshauriwa kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali kwa ajili ya kuongeza chachu ya maendeleo nchini hasa katika sekta ya elimu.

Mwito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi Dar es Salaam jana wakati akizindua Mfuko wa Elimu wa Bonnah.

Alisema mradi kama huo uliobuniwa na Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa kwa ajili ya kusaidia katika sekta ya elimu katika kata hiyo ndiyo miradi inayopaswa kubuniwa na wananchi wengine.

"Hii si kazi ndogo mwenzetu Bonnah alianza na wazo na kisha amethubutu na kuweza kuanzisha mradi huu hakika kila mmoja wetu anakila sababu ya kumpongeza" alisema Mushi.

Alisema kunamaeneo mengi yanayohitaji kusukumwa na si katika sekta ya elimu pekee lakini tunaimani kupitia  mfuko wa elimu wa Bonnah wanafunzi katika  kata hiyo watanufaika nao.


DC Mushi aliwataka viongozi wengine katika maeneo mengine kubuni miradi hiyo jambo litakalo isaidia serikali katika maeneo mengine badala ya kila jambo kufanywa na serikali.

Naye Diwani Bonnah Kaluwa alisema aliamua kuanzisha mfuko huo kwa ajili ya kutoa fursa kwa watoto ambao wazazi wao hawana  kuendelea na masomo badala ya kukaaa nyumbani.

"Mfuko huu ni kwa ajili ya watoto ambao wazazi wao hawatakuwa na uwezo wa kuwasomesha ambao tutawapata kupitia viongozi wanaoishi nao jirani ili kuondoa uwekano wa kuingia mamluki " alisema Kaluwa.

Alisema fedha za mfuko huo zitapatika kutokana kwa wadau mbalimbali wapenda elimu wa ndani na nje ya nchi na kuwa tayari hata baadhi ya mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini  wameonesha nia ya kusaidia kupitia mfuko huo.

"Mfuko huu utaanza kuwanufaisha watoto wa lengwa wa kata hiyo na kadri utakavyokuwa unakua tutajitanua zaidi katika mkoa wa Dar es Salaam hadi nchi nzima lengo likiwa ni kuhakikisha watoto hao wanapata elimu kwa faida ya Taifa la Tanzania" alisema Kaluwa.

Hafla hiyo ya uzinduzi wa mfuko huo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Manispaa ya Ilala, Mstahiki Meya Jerry Silaa, Mbunge wa Ukonga Eugen Mwaiposa, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe wakiongozwa na mkuu huyo wa wilaya hiyo huku ikipambwa na burudani kutoka katika kikundi cha Sanaa cha Safi.

No comments:

Post a Comment