(katikati), akizungumza na Katibu Mtendaji wa
Tume ya Uchumi Afrika (ADF), Dk. Carlos Lopes (wa
pili kushoto), wakati katibu huyo, alipotembelea
wizarani hapo, Dar es Salaam juzi.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi Afrika (ADF), Dk. Carlos Lopes (wa pili kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
WAZIRI wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi Afrika
(ADF), Dr. Carlos Lopes ofisini kwake jumanne asubuhi.
Akizungumzia kuhusu ujio wake, Dk. Carlos alisema chombo
hicho, chenye Makao Makuu yake Adis Ababa kinafanya kazi kwa ushirikiano na
Umoja wa Africa, Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB) na
washirika wengine muhimu katika kuleta maendeleo kupitia programu maalumu za
kimaendeleo.
Carlos alisema tume ya uchumi ina wadau ambao
hufanya midahalo ya kujadili na kuanzisha mikakati madhubuti kwa ajili ya
maendeleo ya Africa.
Alisema, lengo la ADF
ni kuwasilisha matokeo ya utafiti na maoni juu ya masuala muhimu ya maendeleo
ili kuweka malengo, vipaumbele na mipango pamoja na kufafanua mazingira yatakayo
wezesha mataifa ya Afrika kutekeleza programu husika.
Aliendelea kusema mabadiliko makubwa yanatarajiwa kufanyika
katika sekta za madini na nishati na kwamba wanamaono ya kuanzisha kituo cha
maendeleo cha madini (Mining development
centre), kuhamasisha utunzaji wa mali asili pamoja na kuboresha masuala ya kilimo.
Mpango huu huwasilishwa
kwa wadau mbalimbali Afrika wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, watunga sera,
wadau wa maendeleo, taasisi za kimataifa na taasisi zisizo za kiserikali ili
kujadili namna ya kuleta mapinduzi hayo yatakayoinua uchumi wa bara la Africa.
Mheshimiwa Waziri
alimshukuru Dr. Calos kwa kuona umuhimu wa kufika na kuzungumza nae, Mheshimiwa Muhongo alisema amefurahishwa na mpango wa
UNECA (United Nation, Economic Commision for Africa) wa kufanya mabadiliko ya
kiuchumi na kukazia kwamba yuko tayari kushirikiana katika kuleta mabadiliko
hayo. Aidha, Mheshimiwa Muhongo alisisitiza kuwa ni lazima kubadilisha mtazamo wa
baadhi ya waafrika wa kujiona hawawezi kila wakati.
Muhongo alisema
anaamini kwamba Tanzania inaweza kuongoza katika uzalishaji wa madini miaka
ijayo na japo kuwa inakabiliwa na tatizo la uhaba wa wataalamu na mafundi
katika sekta za nishati na madini. Muhongo alisema wataalamu wengi waliopo
wamefikia umri wa kustaafu na hivyo kuacha pengo kubwa kwa tasnia za nishati na
Madini.
Muhongo alisisitiza
umuhimu wa kujenga uwezo wa kitaaluma katika Nyanja za utafutaji na uendelezaji
wa mafuta na gesi aliomba ADF kusaidia
katika kufanikisha suala hilo.
Mpaka sasa Wizara
imejitahidi kutafuta na kupata wafadhili ili kuwawezesha watanzania kujiendeleza katika masuala ya petroli
na gesi katika nchi za Brazili na China na mpaka sasa kuna jumla ya wanafunzi 40. Lakini
pia vyuo mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Technolojia Dar es Salaam na chuo
kikuu cha Dodoma watawezeshwa kutoa mafunzo katika tasnia ya mafuta na gesi.
Waziri aliongeza kwamba
tunahitaji kuongeza uwezo pia katika masuala ya nishati katika maeneo ya
uzalishaji wa umeme, usafirishaji pamoja na usambazaji kwani nishati ni huduma
muhimu ya msingi sana katika kupata maendeleo
No comments:
Post a Comment