TANGAZO


Thursday, March 21, 2013

Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bura, yazuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora, Dk. Pindi Chana (wa tatu kulia), akizungumza na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wakati kamati hiyo, ilipofanya katika ofisi hiyo jana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani (wa pili kulia), akieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Ofisi yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria  na Utawala Bora, walipotembelea ofisini kwake.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu Serikalini, Emmanuel Mlay (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora.

Wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Bora, wakiangalia jinsi Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS), unavyofanya kazi kupitia mtandao katika ziara waliyoifanya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma jana.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (aliyesimama), akiwasilisha kazi za Ofisi yake kwa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora ilipofanya ziara ofisini hapo.

Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora, William Ngeleja (wa pili kulia), akichangia mada wakati wa ziara ya kamati hiyo, katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma)

No comments:

Post a Comment