Mkuu wa Kitengo cha
Wateja Wadogo na wa Kati pamoja na Vicoba wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi
(katikati), akinyanyua mikono na Meneja Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Fair Deal
Auto (PVT), Limited, Anil Dewan (kulia) pamoja na Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Car
& General Trading, Jonathan Masanja, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa benki
hiyo, kuanza kukopesha wateja mikopo ya pikipiki za magurudumu matatu aina ya Bajaj na
Tvs King, kwenye tawi la NMB Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
Mkuu wa
Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati pamoja na Vicoba wa Benki ya NMB, Filbert
Mponzi, akipongezana na Meneja Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Fair Deal Auto (PVT),
Limited, Anil Dewan, wakati wa uzinduzi wa benki hiyo, kuanza kukopesha wateja mikopo ya pikipiki za magurudumu matatu aina ya Bajaj na Tvs King, kwenye tawi la NMB Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam leo.
Na Mwandishi wetu
BENKI ya NMB kwa
kushirikiana na Kampuni ya Fair Deal Auto Private Limited pamoja Car &
General Ltd zinazosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TVS King leo
zimeingia ubia wa kutoa mikopo ya pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaaj na TVS
King kwa bei nafuu zaidi.
Pikipiki hizi zitawawezesha wateja wa NMB kupata
unafuu wa kujikimu kimaisha wakati huo huo wakiendelea na shughuli mbali mbali
za kila siku.
Akizungumza katika uzinduzi huo, uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Wajasiriamali Wadogo na wa kati, Filbert
Mponzi alisema, “Mikopo hii yenye masharti nafuu kabisa, inatolewa kwa mteja
yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Mteja mwenye
nia ya kupata mkopo huu atatakiwa kuwa na uwezo wa kulipia asilimia thelathini
(30%) ya gharama au bei ya Bajaaj au TV’S kama inavyouzwa na wasambazaji wa
pikipiki hizi nchini yaani kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza
pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaj kwa sasa inauzwa kwa Sh. 5,450,000/= na
kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu
aina ya TVS King Ltd inauzwa Sh. 5, 600,000/=”.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa Kati NMB, Filbert Mponzi (kati) Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan (Kulia) na Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja wakifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa wateja wa NMB.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa Kati NMB, Filbert Mponzi (kati) Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan (Kulia) na Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja wakifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa wateja wa NMB.
Mikopo hii ya Bajaj na TVS King kwa sasa inatolewa katika matawi tisa tu ya NMB yaliyopo jijini Dar es Salaam ambayo ni NMB Temeke, NMB Tegeta, NMB Ilala, NMB Airport, NMB Mlimani City, NMB Mwenge, NMB Mbezi, NMB Magomeni na NMB Msasani. Katika siku za usoni NMB ina mikakati ya kutoa huduma hii katika mikoa mingine ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa
NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Masoko wa kampuni ya Car and
General, Jonathani Masanja (pili kushoto) baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za
miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Mauzo wa kampuni
ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.
Mkopo huu unaotolewa kwa muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa taratibu na makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB. Mikopo hii pia inawekewa bima inayomletea unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya asiwe na uwezo wa kufanya shughuli zake za kila siku za kimaisha au kufariki, basi bima hii itachukua jukumu la kumalizia deni la mkopo huu na mteja ataendelea kumiliki pikipiki hii ya miguu mitatu kama kawaida.
Sasa, wateja wa NMB wanaweza kutimiza ndoto zao za kumiliki Bajaj au TVS King kwa kutumia mikopo hii. Benki ya NMB inatoa wito kwa wateja wake kutumia fursa ya kupata mikopo hii kwa unafuu zaidi na kupata fursa ya kumiliki pikipiki hizi za miguu mitatu ili kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment