TANGAZO


Monday, February 25, 2013

Ziara ya Kikazi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya TEHAMA, Priscus Kiwango, wakati alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mfumo shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS), alipofanya ziara ya kikazi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma hivi karibuni, jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi, Micky Kiliba alipokuwa akielezea masuala mbalimbali ya kiutumishi, wakati wa ziara yake, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma hivi karibuni.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia), akipokea nyaraka mbalimbali za kiutumishi kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu, wakati wa ziara yake ya kikazi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma hivi karibuni.


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia), akiongea na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, alipofanya ziara ya kikazi ofisini hapo hivi karibuni.



Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara ya kikazi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma jana.

No comments:

Post a Comment