Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, wakiwa wamebeba maboksi yaliyokuwa na dawa pamoja na vifaa vya tiba, vilivyotolewa na kampuni hiyo, kupitia Vodacom Foundation kwa Zahanati ya Kijiji cha Nyamisati, Rufiji mkoani Pwani juzi. Vifaa hivyo na dawa, vilivyokuwa na tahamani ya sh. milioni 20, vilikabidhiwa kwa mke wa Rais, Mama Salma Kikwete kwa niaba ya zahanati hiyo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom, Matina Nkulu (kushoto), akiyapanga maboksi hayo yaliyokuwa na dawa pamoja na vifaa vya tiba sehemu yalipofanyika makabidhiano hayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Vodacom, akipiga picha pamoja na watoto wa Kijiji cha Nyamisati, yalipofanyika makabidhiano ya dawa na vifaa vya tiba, nje ya Zahanati ya Nyamisati juzi.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Nyamisati wakati alipowasili kwenye Zahanati ya kijiji hicho kwa ajili ya makabidhiano ya dawa na vifaa vya tiba juzi. Vifaa hivyo vilivyotolewa na Kampuni ya Vodacom, kupitia taasisi yake ya huduma za jamii ya Vodacom Foundation.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akisalimiana na wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, wakati alipowasili kijijini hapo kwa ajili ya makabidhiano ya dawa na vifaa vya tiba kusaidia Zahanati ya Nyamisati, Rufiji, mkoani Pwani juzi. Vifaa hivyo na dawa, vyenye thamani ya sh. milioni 20, vilitolewa na Kampuni ya Vodacom, kupitia taasisi yake ya huduma za jamii ya Vodacom Foundation.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo, wakati alipowasili kijijini hapo kwa ajili ya makabidhiano ya dawa na vifaa vya tiba, kusaidia Zahanati ya Kijiji cha Nyamisati, Rufiji, mkoani Pwani juzi. Vifaa hivyo na dawa, vyenye thamani ya sh. milioni 20, vilitolewa na Kampuni ya Vodacom, kupitia taasisi yake ya huduma za jamii ya Vodacom Foundation.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo, wakati alipowasili kijijini hapo kwa ajili ya makabidhiano ya dawa na vifaa vya tiba, kusaidia Zahanati ya Kijiji cha Nyamisati, Rufiji, mkoani Pwani juzi. Vifaa hivyo na dawa, vyenye thamani ya sh. milioni 20, vilitolewa na Kampuni ya Vodacom, kupitia taasisi yake ya huduma za jamii ya Vodacom Foundation.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, wakati alipowasili kijijini hapo kwa ajili ya makabidhiano ya dawa na vifaa vya tiba kusaidia Zahanati ya Kijiji cha Nyamisati, Rufiji, mkoani Pwani juzi. Vifaa hivyo na dawa, vyenye thamani ya sh. milioni 20, vilitolewa na Kampuni ya Vodacom, kupitia taasisi yake hiyo ya huduma za jamii ya Vodacom Foundation. Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtingwa.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akizungumza na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha Rose Migiro (kulia), mara baada ya kuwasili katika hafla ya makabidhiano hayo, Kijiji cha Nyamisati, Rufiji mkoani Pwani. Kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule.
Wananchi wa Kijiji cha Nyamisati, Rufiji mkoani Pwani, wakifurahia jambo kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtingwa.
Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kulia), akimkabidhi baadhi ya dawa na vifaa vya tiba, vyenye thamani ya sh. milioni 20, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, ikiwa ni msaada kwa ajili ya Zahanati ya Kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani. Kushoto anayemsaidia mama Kikwete ni Ofisa Tabibu wa zahanati hiyo, Haroun Zuberi.
Wananchi wa Kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, wakimsikiliza mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, alipokuwa akiwahutubia katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akihutubia wakati wa hafla hiyo, kijijini hapo juzi mara baada ya kukabidhiwa dawa na vifaa vya tiba na Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akipiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, mara baada ya kumaliza kuhutubia katika hafla ya makabidhiano hayo, kijijini hapo. Wa pili kulia ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha Rose Migiro na watatu ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom, Rukia Mtingwa.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu (katikati), akipiga picha ya pamoja na wazee wa Kijiji cha Nyamisati pamoja na wafanyakazi wa Vodacom, mara baada ya makabidhiano hayo. Wa pili kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtingwa.
No comments:
Post a Comment