Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiwania mpira na beki wa Kagera Sugar, Benjamini Asukile, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Katika mchezo huo, Yanga imeshinda bao 1-0 na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kukaribia kuunyakua Ubingwa wa ligi hiyo.
Beki wa Yanga, Nadir Haroub Canavaro, akiwatoka wachezaji wa Kagera Sugar katika mchezo huo.
Wachezaji wa Kagera Sugar, wakimlalamikia mwamuzi msaidizi wa mchezo huo, Milambo Tshikungu kutoka Mbeya.
Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto), akichuana na Daudi Jumanne wa Kagera Sugar. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto Blog)
No comments:
Post a Comment