TANGAZO


Thursday, February 28, 2013

Waziri Mkuu Pinda, azindua mpango mkakati wa GS1 Tanzania

Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho cha GS1 Tanzania, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Makamu Mwenyekiti wa GS1 Tanzania, Yakub Hasham akizungumza na wadau  mbalimbali waliohudhuria kikao cha tatu cha washika dau na kikao cha pili cha mwaka cha GS1 Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo akifafanua jambo juu ya umuhimu wa Barcodes katika kuinua soko la bidhaa nchini.
Salum Awadh, akiwasilisha  mpango mkakati wa GS1 Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2013-2018 kama Mtaalamu Mshauri ( Consultant) wa GS1 Tanzania.
Mwenyekiti wa Amsha Institute of Rural Entrepreneur, Biubwa Ibrahim Malengo, akizungumzia mafanikio ya kikundi chake hicho, kutoka Lindi Vijijini.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua kikao cha tatu cha washika dau katika Hotel ya Blue Pearl, Ubungo Plaza leo, Feb 27, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia washika dau wa GS1 Tanzania, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango mkakati wa GS1 Tanzania kwa miaka 5.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akionyesha kwa washika dau, mpango mkakati aliouzindua leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akikata keki, mara baada ya kuuzindua mpango mkakati wa GS1 jijini leo. 
Wajumbe kutoka Zanzibar,  wakifuatilia kwa makini yanayojiri kwenye kikao cha tatu cha washika dau na kikao cha pili cha mwaka cha GS1 Tanzania
Mjasiriamali, Faith Temba wa kampuni ya FANO 2010, akipokea barcodes ya bidhaa zake. Jumla ya  wafanyabiashara wa  asali wapatao 10, wamekabidhiwa barcodes zao leo, jijini wakati wa kikao cha tatu cha washika dau na kikao cha pili cha mwaka cha GS1 Tanzania. (Picha zote na Adam Mzee)

No comments:

Post a Comment