TANGAZO


Thursday, February 21, 2013

Rais Mwai Kibaki wa Kenya azindua barabara ya jina lake, Dar es Salaam


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakiongozwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yusuph  Mwenda, kutembea hatua chache kabla ya kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013, kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo. (Picha zote na Ikulu) 



Rais Mwai Kibaki wa Kenya akikata utepe, akishuhudiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda, kuzindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013.



Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yussuf Mwenda, akizindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013

Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifurahi pamoja na mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda, baada ya kuzindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, makutano ya barabara za Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam, leo Februari 21, 2013.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya akimpa mkono mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kuzindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam, leo Februari 21, 2013. Wengine kulia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda.

Sehemu ya barabara iliyopewa  rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, inavyoonekana maeneo ya makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013.

Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, wakiwa katika hafla hiyo.

Wanamuziki wa bendi ya Vijana Jazz, wakitumbuiza wakati wa uzinduzi rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, maeneo ya makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda, akimkaribisha Rais Mwai Kibaka na Mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika uzinduzi  rasmi wa  jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo katika hafla iliyofanyika makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013.

Sehemu palipoandaliwa kwa uzinduzi  rasmi wa  jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, maeneo ya makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda akimkabidhi zawadi ya kasha la Zanzibar, Rais Mwai Kibaki huku Mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia katika uzinduzi  rasmi wa jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, maeneo ya makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda akimkabidhi zawadi ya kasha hilo kutoka Zanzibar kwa Rais Mwai Kibaki huku Mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia, wakati wa uzinduzi  rasmi wa jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, maeneo ya makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda akimpa mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mara baada ya kumkabidhi Rais Mwai Kibaki zawadi ya kasha la Zanzibar, wakati wa uzinduzi  rasmi wa jina la Barabara ya Mwai Kibaki, linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo, maeneo ya makutano ya barabara za Bagamoyo, Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo, Dar es Salaam leo, Februari 21, 2013.

No comments:

Post a Comment