Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa hafla hiyo maalumu, iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo, Februari 24, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa hafla hiyo maalumu, iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo, Februari 24, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa hafla hiyo maalumu, iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo, Februari 24, 2013.
Rais Paul Kagame (wa tatu kuli) wa Rwanda akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa hafla hiyo maalumu, iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo, Februari 24, 2013.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa, Dk. Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma (wa pili kulia), akisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa hafla hiyo, maalumu iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia leo, Februari 24, 2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (nyuma), akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa hafla hiyo, maalumu, iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mjini, Addis Ababa, Ethiopia leo, Februari 24, 2013.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim na wajumbe wengine wa ujumbe wa Tanzania wakiwa katika ukumbi wa mkutano, wakati wa uwekaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia leo, Februari 4, 2013.
Rais Joseph Kabila (kushoto) wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda, wakibadilishana mawazo kwa furaha, huku Rais wa Jamhuri ya Kongo (Brazaville), Denis Sassou Nguesso, akiwa kati yao baada ya wote kweka saini katika Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati wa hafla hiyo, maalumu iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia leo, Februari 4, 2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (katikati mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu baada ya uwekaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa hafla hiyo, maalumu iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia leo, Februari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akipongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kwa kuwa mmoja wa viongozi wa bara la Afrika, walio mstari wa mbele kusimamia amani baada uwekaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia leo, Februari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akipongezana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn baada uwekaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia leo, Februari 4, 2013. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dk. Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma. (Picha zote na Ikulu)
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Februari 24, 2013 ameungana na Wakuu wenzake wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kutia saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Rais Kikwete alisema mara baada ya utiwaji saini wa Mpango huo kwamba: “Hii ni siku kubwa na ya kihistoria kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jirani zake na Ukanda wote wa Maziwa Makuu. Ni siku ya kukumbukwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Afrika, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya yote ya Kimataifa.
“Watu wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu sana. Wanastahili kupumua sasa. Wanastahili kuishi maisha bora; maisha ambayo usalama wao umehakikishiwa na kuthibitishwa; maisha ambayo yatawafanya waendeshe maisha yao kwa kufanya mambo ya maana zaidi katika kuboresha maisha yao ya kila siku.
“Saini tulizotia kwa Mpango huo leo ni kielelezo cha dhati na ahadi ya utekelezwaji wa yale yanayotarajiwa na watu wa Kongo na Ukanda wa Maziwa Makuu kwa ajili ya Amani, Usalama na Ushirikiano.
“Kwa niaba ya Serikali na Watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naahidi kwamba sisi tutatekeleza kwa dhati yale yote yanayotarajiwa kwa upande wetu”, alisema.
Mpango huo una nia ya kuchangia juhudi ambazo zimefanywa na ICGLR na SADC katika kutafuta amani Mashariki ya Kongo na ukanda wote wa Maziwa Makuu kwa ujumla.
Mpango huo pia umetilia maanani mapendekezo muhimu yaliyokubalika baada ya mashauriano kati ya wakuu wa nchi za ICGLR na SADCna Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mapendekezo ya mpango huo ni pamoja na kuboresha sekta ya Ulinzi na usalama, hususan jeshi la polisi, Kuimarisha mamlaka ya nchi hasa mashariki ya Kongo; na kuendeleza ajenda kuhusu maelewano, kuvumiliana na kudumisha demokrasia nchini humo.
Vile vile, nchi za Kanda zimetakiwa kutoingilia mambo ya ndani ya nchi jirani, kututoa msaada wowote wa vikundi vya waasi, kuheshimu utawala na maeneo ya nchi jirani na kuimarisha mahusiano ya Kanda.
Hali kadhalika, Jumuiya ya Kimataifa imetakiwa kuisaidia DRC na Kanda yote ya Maziwa Makuu kwa ujumla katika utekelezaji wa miradi muhimu pamoja na mkataba wa Amani, Usalama na Maendeleo katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Aidha, Mpango huo unapendekeza kuwepo kwa chombo cha usimamizi (Oversight Mechanism) ambacho kitaundwa na viongozi wote wa nchi 11 pamoja na Umoja wa Mataifa, SADC na ICGLR.
Imetolewa na:
Muhidin Issa Michuzi,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Addis Ababa,
ETHIOPIA.
24 Februari, 2013
No comments:
Post a Comment