TANGAZO


Friday, February 1, 2013

Rais Jakaya Kikwete, akamilisha Usajili wa Kitabulisho cha Taifa, akutana na Makamu wa Rais mstaafu wa Benki ya Dunia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake asubuhi ya leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini baada ya  kuthibitisha maelezo yake binafsi kwenye fomu ya Kitambulisho cha Taifa, wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa kitambulisho hicho,  nyumbani kwake, jijini Dar es salaam leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson E Maimu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akichukuliwa alama za vidole, wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, nyumbani kwake, asubuhi ya leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akiagana na Makamu wa Rais mstaafu wa Benki ya Dunia, Justin Yifu Lin,  leo Ijumaa, Februari mosi, 2013, Ikulu, jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Balozi wa China katika Tanzania, Lu Youqing. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment