TANGAZO


Thursday, February 14, 2013

Matukio mbalimbali ya Mkutano Mkuu wa Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema (kushoto), akimkabidhi Hati ya Kata bora kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa kutumia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman kwa niaba ya Kata ya Isansa na Tarafa ya Igamba zote za Mkoani Mbeya ambazo zimezawadiwa kila moja Hundi ya Shilingi Milioni moja juzi mjini Dodoma. (Picha zote na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Ali Mwema akitoa  mada kwenye Mkutano Mkuu wa Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa Pius Msekwa.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange, akitoa  mada kwenye Mkutano Mkuu wa Maofisa Makuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa Pius Msekwa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema (kushoto), akimkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Visiwani Zanzibar, Kamishna Msaidizi, Aziz Juma Mohamed, mfano wa hundi ya shilingi milioni moja ya Jimbo la Mji Mkongwe, ambalo limekua bora kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa kutumia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi kwa kipindi cha Mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment