TANGAZO


Thursday, February 28, 2013

Marekani yatoa msaada kwa waasi Syria


Mashauriano kuhusu mpango wa kusaida waasi Syria
Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ametangaza kuwa nchi yake itawapa wapinzani wa Rais Bashar al Assad msaada wa zana za kivita zenye thamani ya dola milioni 60.
Waziri Kerry ametoa ahadi hiyo mara tu baada ya mkutano wa marafiki wa waasi wa Syria kumalizika huko mjini Roma.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa marekani kusaidia waasi tangu waanzishe hararakati za kumuondoa Rais Assad Madarakani.
Bwana Kerry ameashiria kuwa huenda sera ya Marekani ibadilike na kuna ripoti ya kuwepo vile vile mpango wa kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wapiganaji waasi, ukijumuisha vyakula na matibabu.

No comments:

Post a Comment