![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVaoPkd1_KnbWiVrzDNyou6gVyb2BEf4YZq6ST5uegA1VwDdTInuWDQ245Njn4kCvTr-VCesl66QRoXJUd12rDGcb9IhtawW6W3-Jbpf0S-K-W16BEqwDP_70cyz_FyRXXcFg6_qhjna9F/s640/tume1.jpg)
Jaji Mkuu wa Kenya, Willy Mutunga (katikati), akibadishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Sengondo Mvungi nje ya Ukumbi wa Tume jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo, Ijumaa, Feb. 15, 2013. Mutunga alikutana na Wajumbe ili kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba Mpya. (Picha zote na Tume ya Katiba)
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani (kushoto), akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Kenya, Willy Mutunga, nje ya Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume hiyo, leo Ijumaa, Feb. 15, 2013. Mutunga amekutana na Wajumbe wa Tume ya Katiba ili kubadilishana mawazo na uzoefu wake, kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto), akimwonesha nakala ya Kitabu, Jaji Mkuu wa Kenya, Willy Mutunga (katikati), nje ya Ofisi za Tume, mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wajumbe wa Tume baina yao, uliofanyika katika Ofisi za Tume, jijini Dar es Salaam leo, Ijumaa Feb. 15, 2013. Mtungi amekutana na Wajumbe wa Tume hiyo, ili kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba.
No comments:
Post a Comment