Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Ahmed Seif Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 6,040 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (hayupo pichani), jijini leo. Katibu Mkuu msaidizi wa TASWA, George John.
Katibu Mkuu msaidizi wa TASWA, George John, akizungumza katika mkutano huo, wakati alipokuwa akiishukuru Kampuni hiyo kwa msaada huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Ahmed Seif Mohamed.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Ahmed Seif Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 6,040 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando na katikati ni msaidizi wake, George John.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Ahmed Seif Mohamed (wa pili kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 6,040 Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando (kulia), kwa ajili ya kusaidia Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Na Kassim Mbarouk
Kampuni ya Simu ya Zantel imesema kuwa wao kama wadau wakubwa wa kusaidia mambo ya michezo nchini wanayofuraha ya kutangaza kusaidia kuunga mkono kwa kusaidia Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), utakaofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani Disemba 21 hadi 22, mwaka huu.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, wakati akikabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 6,040 kwa TASWA, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni hiyo, Ahmed Seif Mohamed, alisema kuwa wanaamini kuwa Waandishi wanamchango mkubwa kwa maendeleo ya michezo na kwa hivyo ndiyo maana kampuni yake ikahisi kwamba ni muhimu kuusaidia mkutano huo.
"Zantel ni mdau wa michezo katika nchi hii. Tunaweza kuelezea mengi kuhusu hilo, lakini shindano lililomalizika hivi karibuni la Epiq BSS linaweza kuwa moja ya mifano hiyo", alisema Mohamed.
Aidha, alisema kuwa wataendelea kudhamini shindano hilo kwa mwaka ujao na kuthibitisha nia yao ya kukuza vipaji nchini, na kuongeza kuwa wataendelea kusaidia mashindano hata baada ya kumalizika kwake.
"Tunaendelea kurekodi nyimbo za washindi wote 12 wa nafasi za juu na mshindi atasaidiwa kurekodi albuma nzima na kupata udhamini wa mwaka nzima", alisema.
Alisema kuwa wamataarifiwa na Katibu Mkuu kwamba mkutano huo utawapatia waandishi wa michezo ubadilishanaji mawazo na kujadili mambo mbalimbali katika nyanja za michezo na kuongeza kwamba kwa sababu hizo pekee wanahisi kuwa ni sababu kubwa ya kusaidia mkutano huo.
Aliongeza kuwa msaada huo ni mfano wao wa kuunga mkono na kuthamini mchango wa habari kuelekea kwenye mafanikio ya kampuni na jamii kwa jumla.
Alisema kuwa kampuni yao imetangazwa kuongoza katika soko na Tume ya Mawasiliano nchini (TCRA) katika ripoti yake ya robo mwaka kwa ongezeko la 17% la wateja na kwa hivyo alisema kuwa wanaamini kuungwa kwao mkono na jamii ndiko kulikoleta mafanikio hayo.
Na mwisho, alifungua milango ya kampuni hiyo kwa wadau wate wa michezo kwamba wao, Zantel kuwaona watakapokuwa na mahitaji na msaada wowote na kuutakia mafanikio mkutano huo, utakaofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment