TANGAZO


Thursday, December 13, 2012

Mbatia, Cheyo wawatetea wafugaji wa Morogoro kutokana na dhuluma wanazodai kufanyiwa na uongozi wa mkoa huo

 Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu dhuluma wanazofanyiwa wafugaji na utawala wa Mkoa wa Morogoro, ambapo alielezea kuwa umekuwa ukiwatoza fedha nyingi wafugaji kinyume na sheria na kuwataka kuhama maeneo ya mkoa huo na kurudi maeneo yao ya asili walikotoka. Mbatia aliutaka uongozi wa Mkoa huo kurejesha fedha hizo kwa wafugaji hao na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati suala hilo alilodai kwamba ni dhuluma kwa wafugaji hao na pia kuutaka uongozi huo kuacha zambi za kubaguana kwa umajimbo na kuongeza kuwa hata yeye Mkuu wa Mkoa huo, Morogoro sio kwao naye arudi kwao Korogwe. Pia alisema watu wa Morogoro pekee hawawezi kukufikisha Ikulu kama unagombea Urais, amewataka viongozi hao kuacha mara moja tabia hiyo kwani itasababisha uvunjifu wa amani na kutolea mfano Mkoa wa Dar es Salaam kwamba wenyeji wa mji huo ni Wazaramo nao wakiamua kuwafukuza wengine basi hapatabaki mtu na hatimaye kuwa fujo na vurugu chi nzima. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo, ambaye wameshirikiana kuwaunga mkono na kuwatetea wafugaji hao. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu dhuluma wanazofanyiwa wafugaji na utawala wa Mkoa wa Morogoro, ambapo alielezea kuwa umekuwa ukiwatoza fedha nyingi wafugaji kinyume na sheria ambapo alisema pia kuwa uongozi wa mkoa huo, umewataka kuhama maeneo hayo na kurudi maeneo yao ya asili walikotoka.

Baadhi ya waandishi wa habari, wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia, wakati wa mkutano huo wa kuwatetea wafugaji wa Mkoa wa Morogoro kutokana na dhuluma wanazofanyiwa na utawala wa mkoa huo, ambapo alisema kuwa umekuwa ukiwatoza fedha nyingi wafugaji kinyume na sheria ambapo alisema pia kuwa uongozi wa mkoa huo, umewataka kuhama maeneo hayo na kurudi maeneo yao ya asili walikotoka.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu dhuluma wanazofanyiwa wafugaji na utawala wa Mkoa wa Morogoro, ambapo alielezea kuwa umekuwa ukiwatoza fedha nyingi wafugaji kinyume na sheria ambapo alisema pia kuwa uongozi wa mkoa huo, umewataka kuhama maeneo hayo na kurudi maeneo yao ya asili walikotoka.

Waandishi waandamizi Eben-ezer Mende wa Jambo Leo (kushoto) na Bakari Kimwanga wa Mtanzania wakiandika habari zilizokuwa zikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu dhuluma wanazofanyiwa wafugaji na utawala wa Mkoa wa Morogoro, ambapo alielezea kuwa umekuwa ukiwatoza fedha nyingi wafugaji kinyume na sheria na kuwataka kuhama maeneo ya mkoa huo na kurudi maeneo yao ya asili walikotoka.

Mwenyekiti wa Chama UDP, John Cheyo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu dhuluma wanazofanyiwa wafugaji na utawala wa Mkoa wa Morogoro, ambapo yeye pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia (kushoto kwake aliyefichika), walielezea kuwa uongozi huo, umekuwa ukiwatoza fedha nyingi wafugaji kinyume na sheria ambapo walisema pia kuwa uongozi wa mkoa huo, umewataka kuhama maeneo hayo na kurudi maeneo yao ya asili walikotoka.

Mwenyekiti wa Chama UDP, John Cheyo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu dhuluma wanazofanyiwa wafugaji na utawala wa Mkoa wa Morogoro, ambapo yeye pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia (kulia), walielezea kuwa uongozi huo, umekuwa ukiwatoza fedha nyingi wafugaji kinyume na sheria ambapo walisema pia kuwa uongozi wa mkoa huo, umewataka kuhama maeneo hayo na kurudi maeneo yao ya asili walikotoka.

Mmoja wa wafugaji wa Mkoa wa Morogoro, Wilson Limbu (kulia), aliyedai kufanyiwa dhuluma hizo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama UDP, John Cheyo na katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo na  kulia ni mmoja wa wafugaji wa Mkoa wa Morogoro, wanaodai kufanyiwa dhuluma hiyo, Wilson Limbu.

No comments:

Post a Comment