Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, akipatiwa maelezo na mtalamu wa Tanesco Makao Makuu Eng.
Tumaini Temu kuhusu jinsi jenereta walilolifunga linavyofanya kazi katika
kuzalisha umeme katika kijiji cha Kibaoni. kushoto kwa Waziri Mkuu ni tekinisheni
wa Tanesco Bibi.Salama Mpera.
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, akikagua kibanda kilichojengwa kwa ajili ya kuweka jenereta la kufua umeme katika kijiji cha Kibaoni, Katavi. Waziri Mkuu yupo katika ziara ya
kukukagua shughuli za maendeleo na mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya kijijini
kwao, Kibaoni Katavi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwa katika shamaba lake
katika kijiji cha Kibaoni, Katavi akiangalia mahindi
yalivyostawi.
Godfrey Pinda, ambaye
ni mdogo wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akimwelezea Waziri Mkuu kuhusu
anavyolima kilimo cha mananasi na minazi katika shamba lake kijijini
Kibaoni, Katavi. Waziri Mkuu yupo katika jimbo lake la Katavi katika kukagua
shughuli za maendeleo pamoja na mapumziko ya Krismasi na mwaka
mpya. (Picha
zote na Chris Mfinanga)
No comments:
Post a Comment