TANGAZO


Sunday, December 30, 2012

Vijana jijini Dar es Salaam wahamasishwa kufanya mazoezi kuimarisha afya

 

 
Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzani, akiwapa mazoezi vijana wa Klabu za Jogging 12 za maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakati alipoalikwa kushiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini. Kabla kuanza bonanza hilo, kulikuwa na mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilometa 8, kutoka Kawe kupitia Lugalo hadi Mbezi Beach na kurejea kwa kupita barabara ya Bagamoyo ya zamani hadi. (Picha zote kwa hisani ya Said Powa)
 
 
Pamoja na kuwepo kwa mvua vijana hao hawakuacha kufanya mazoezi.
 
 
Vijana wa jiji la Dar es Salaam kutoka kwenye Klabu za Jogging zipatazo 12, wakifanya mazoezi ya kukimbia mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa Bonanza la kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013, lililoandaliwa na Klabu ya Jogging ya Kawe jijini.
 
 
Vijana wa Klabu za Jogging zipatazo 12, wakifanya mazoezi ya kukimbia mapema leo, asubuhi jijini Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa Bonanza la kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013, lililoandaliwa na Klabu ya Jogging ya Kawe jijini.
 
 
Mbunge Iddi Azzani, akiongoza mazoezi ya kunyoosha viungo na vijana kwenye bonanza hilo.

No comments:

Post a Comment