Msanii wa maarufu wa muziki wa dansi kutoka nchini Zaire, JB Mpiana akiingia katika viwanja vya Leaders Club jana usiku mida ya saa tisa kasoro, kuanza shoo baada ya kuchelewa kupanda kutokana na umeme kuzingua, huku bendi ya Mashujaa ikishindwa kuzindua rasmi albam yake ya Risasi Kidole.
JB Mpiana, akipanda jukwaani kuanza kushambulia jukwaa.
JB Mpiana, akianza kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi viwanjani hapo, akiwa na wanenguaji wake.
Mashabiki wakishangilia na kupata kumbukumbu kupitia simu zao za mkononi.
Sebene lilianza kuchanganya kama hivi.....huku Rapa wa bendi hiyo akikamua.....
Rapa wa bendi hiyo akiwangoza wanenguaji wake kushambulia jukwaa.
Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa, Chalz Baba, akiingia uwanjani hapo akiwa na Trekta, ikiwa ni staili yake ya kuingia ukumbini hapo, ambayo hata hivyo alishindwa kulitumia Trekta hilo kuwaonyesha mashabiki wake, kutokana na kuzinguliwa na umeme.
Chalz Baba, akishuka katika Trekta lake kuingia katika shoo hiyo.
Mtangzaji wa EATV, Patrick Nyembela, akiwa na wadau wakifuatili uzinduzi huo...
William Malecela (kushoto) akiwa na Juma Pinto (katikati) na Ben Kisaka, wakiwasili katika uzinduzi huo.
Njiwa naye alikuwapo kufikisha salam za uzinduazi huo.
Wanenguaji wa Mashujaa Band, wakikamua jukwaani wakati wa shoo ya ufunguzi wa uzinduzi wa albam yao, ambao shoo hii waliicheza jukwaani bila kumalizika kutokana na matatizo ya umeme.
'Mkaanga Chips' wa Mashujaa, akizicharaza Drams.
Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiingia kwa staili yao ya kucheza muziki wa Kihindi, wakati wa shoo yao ya pamoja, ambayo hata hivyo haikuweza kumalizika.
Wanenguaji wa Mashujaa, wakikamua jukwaani..
Makamuzi yakiendelea..
Shoo ilikuwa ni tamu kwa kweli, lakini haikuwa na raha kutokana na karaha ya umeme.
Mpiga Tumba wa bendi hiyo, MCD akizicharaza tumba....
Sehemu ya mashabiki wa VIP waliolipa kiingilio cha Sh. 100, 000 kila mmoja, wakiwa katika eneo lao la VIP.
Gari alilolitumia JB Mpiana kuingia uwanjani hapo......
Mafundi mitambo, wakishangaa wasijue la kufanya baada ya kukatika kwa umeme huo kila muda.
Mtangazaji Ben Kinyaiya, akifanya mahojiano na Jado Fidifosi wakati wakiendelea kulazimisha shoo hiyo.
Ben Kinyaiya naye akisebeneka..
Mnenguaji wa Mashujaa, akikamua.
Rapa wa Bendi ya Mashujaa, Ferguson, akiwachezesha wanenguaji wake.....kwa rap ya 'Kibega'
Ni Nyuzi bin Nyuzi hapa.......
Mafundi wakihaha kurekebisha Jenereta baada ya kuzingua.......
Sehemu ya mashabiki, wakisebeneka.....
Wanasa matukio nao hawakuwa nyuma katika kazi yao......
Kazi na dawa, Paparazi huyu baada ya kuchenguka vilivyo na sebene la JB, ilibidi kusahau kazi na kuamua kusebeneka.
VIP.......
Huyu naye alinaswa na kamera yetu, si mwingine bali ni mzee wa Mtaa kwa Mtaa Blog, Othman Michuzi, akisebeneka.
Mkaanga chips wa JB, akizicharaza Drams..... (Picha zote na mtandao wa www.sufianimafoto.blogspot.com)
BENDI ya Wenge BCBG usiku wa kuamkia leo ilikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliofika kwenye viwanja vya Leaders Club kushuhudia uzinduzi wa albam ya pili ya Bendi ya Mashujaa ya Risasi Kidole, huku matatizo ya kiufundi yakisababisha bendi ya Mashujaa kushindwa kuzindua albamu hiyo.
Pamoja na kuchelewa kuanza kwa shoo hiyo, kutokana na matatizo ya kukatika kwa umeme kila muda, JB Mpiana alianza kuwatanguliza wanamuziki wake wakiongozwa na mmoja wa waanzilishi wa bendi hiyo, Shai Ngenge, na kupiga sebene kabambe kabla ya kufuatiwa na wimbo wa zamani wa Kinie Bouger,ambao enzi zake alishirikiana na akina, Ngiana Makanda, miaka ya katikati ya 1990.
Wimbo huo uliweza kuondoa kero kwa mashabiki hao na kuwasahaulisha yale yaliyokuwa yakiwatokea wanamuziki wa Mashujaa, ambao kila walipokuwa wakipanda jukwaani na wanapofika kuanza sebene umeme unakatika, jambo lililowafanya kupanda jukwaani mara nne, lakini wakishindwa kumaliza wibo mmoja tu wa Risasi Kidole.
JB Mpiana alionekana kuwa ni mkombozi kwa mashabiki wachache waliokuwa wamebaki huku wakipiga moyo konde kuwa hawataondoka viwanjani hapo bila ya kumuona JB, katika uzinduzi huo kutokana na burudani safi.
Kitu ambacho kiliwashangaza mashabiki wengi ni kutokatika kwa mara kwa mara kwa umeme kama ilivyotokea kwa bendi ya Mashujaa ilipokuwa jukwaani.Mpiana aliweza kufanya kweli katika shoo hiyo kwani umeme haukukatika mpaka aliposhuka jukwaani majira ya saa 10 alfajiri.
Katika shoo hiyo, Mpiana aliweza kupiga nyimbo mbali mbali za zamani ikiwa pamoja na Barakuda, Djodjo Ngonda, Walay Danico, Dizo Dizo na zile mpya katika mtindo wa non-stop.
Mashujaa ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na mara walipoanza kucheza shoo ya ufunguzi ambao imewajumuisha wanenguaji wa kike na wa kiume na waimbaji, umeme ulikatika na kazi ya kuanza kurejesha ikaanza na kuchukua muda wa dakika zisizopungua 30.
Tatizo hilo liliendelea mara kwa mara huku bendi hiyo ilishindwa kumaliza tatizo hilo na jitihada za kutatua hazikutoa jibu la mara moja, huku Mmoja wa viongozi wa Bendi hiyo, King Dodoo, akionekana kuhaha kila kona ya uwanja huo akiwa na Babu aliyekuwa akijitahidi kusoma dua ili Jenereta hilo liweze kufanya kazi bila kusumbua.
Mafundi walijitahidi sana na mara baada ya mashabiki kutaka JB Mpiana apande, mafundi walitatua tatizo hilo na kumwezesha mwanamuziki huyo kufanya shoo bila tatizo hadi alipomaliza ratiba yake.
Katika tukio jingine lililojitokeza viwanjani hapo ni Mkurugenzi wa bendi hiyo, Mama Sakina, aliyeanguka ghafla, ikieleza ni presha ya ghafla kutokana na kile kilchokuwa kikiendelea mahala hapo na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment