Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, James Kajugusi (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza, Makoye Bunoro, sh. 50,000/- kwa ajili ya kuweka mafuta katika pikipiki za kitengo cha Polisi Jamii pale wanapoenda kupambana na wahalifu. Umoja huo unawasaidia waendesha pikipiki 2034, kupata leseni na mafunzo yanayotolewa na Chuo cha VETA kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, James Kajugusi (kulia), akiongea jambo hivi karibuni na viongozi Chama cha Umoja wa Wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza (hawapo pichani), alipowatembelea ofisini kwao, eneo la Mlango Mmoja, ili kuangalia shughuli zinazofanywa na umoja huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja huo, Makoye Bunoro.
Mdhibiti wa mali za Chama cha Umoja wa Wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza, Faraji Abdalah (kushoto), akimwelezea jambo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, James Kajugusi (kulia), jinsi umoja huo, ulivyoweza kuunda kitengo cha Polisi Jamii ambacho kinashirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja huo, Makoye Bunoro.
Viongozi wa Umoja wa Wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, James Kajugusi (hayupo pichani), akiwaeleza jinsi wanavyoweza kuunda SACCOS yao na kukopa fedha kutoka Mfuko wa vijana ambazo zitawasaidia kununua pikipiki zao na kujiajiri wakati alipowatembelea ofisini kwao, ili kuangalia shughuli zinazofanywa na umoja huo. (Picha zote na mdau wetu)
No comments:
Post a Comment