Mhitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal, Mary Yuda, akifurahia jambo, wakati wa mahafali ya 11 ya chuo cha hicho, yaliyofanyika Manzese, Dar es Salaam juzi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal, wakipwa katika mahafali yao ya 11, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba (hayupo pichani), katika mahafali yaliyofanyika Manzese, Dar es Salaam juzi.
Mhitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal, Mary Yuda, akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba.
Grace Kingalame Kihampa (kushoto), akimpongeza kwa busu mfanyakazi mwenzake wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Agness Mbapu, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uandishi wa habari katika Chuo cha Uandishi wa habari cha Royal, Dar es Salaam juzi.
Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Agness Mbapu, akipozi kwa picha na mtoto wa dada yake, Julian baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uandishi wa habari katika Chuo cha Uandishi wa habari cha Royal, Dar es Salaam juzi.
Grace Kingalame Kihampa (wa pili kushoto), akimpongeza na kumpa maua mfanyakazi mwenzake wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Agness Mbapu, baada ya kuhitimu na kutunukiwa Stashahada ya Uandishi wa habari katika Chuo cha Uandishi wa habari cha Royal, Dar es Salaam juzi.
Mhitimu wa Chuo cha uandishi wa habari cha Royal, Mary Yuda akipongozwa kwa kupewa shada la maua na ndugu yake, Janet Mosha (kulia), wakiti wa mahafali ya 11 ya chuo hicho, Manzese, Dar es Salaam juzi. Wengine pichani ni kaka zake Mary Yuda.
Mhitimu, Mary Yuda akipongozwa kwa kupewa shada la maua na Janet Mosha (kulia), wakiti wa mahafali hayo ya 11 ya chuo hicho, Manzese, Dar es Salaam juzi. Wengine pichani ni kaka zake Mary Yuda.
Grace Kingalame Kihampa (kushoto), akimpongeza kwa busu lenye tabasamu, rafiki yake, mfanyakazi wa Magazeti ya Kampuni ya Mwananchi (MCL), Oliva Albert, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uandishi cha Royal, Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada katika Chuo cha uandishi wa habari cha Royal, wakiwa kwenye mahafali yao ambayo mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba (hayupo pichani), aliwakabidhi vyeti vyao vya kuhitimu, Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunukiwa vyeti vyao na mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba (nyuma yao pichani), Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada katika Chuo cha Uandishi wa habari cha Royal kutoka Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba (hayupo pichani), katika mahafali ya 11 ya Chuo hicho, Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada katika Chuo cha Uandishi wa habari cha Royal kutoka Zanzibar, wakipongezana baada ya kutunukiwa vyeti vyao na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba (hayupo pichani), katika mahafali ya 11 ya Chuo hicho, Dar es Salaam juzi.
Mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal, Sophia Augustino, akikonga nyoyo za wahitimu na wageni mbalimbali waliofika katika mahafali hayo ya 11, kwa kuwaporomoshea ngoma nzito za kisasa katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba.
No comments:
Post a Comment