Bendi za musiki wa dansi zinazotumia miondoko ya Ndombolo ya Solo, za Twanga Pepeta na Diamond Musica usiku wa kumkia leo, zilifunika na kukonga nyoyo za mashabiki wa Muziki huo, mjini Moshi, wakati wakali hao wawili walipotumbuiza katika Tamasha kubwa la burudani la 'Tusker Carnival', lililofanyika katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Walikuwa ni Diamond Musica, walioanza kulishambulia jukwaa hilo la Tusker Carnival, mishale ya saa mbili usiku hadi sita kasorobo, walipo wapisha wenzao, wakongwe wa burudani na wabishi wa mjini, Twanga Pepeta, ambao wautikisa vilivyo mji wa Moshi.
Tamasha hilo la Tusker Carnival, lilianza juma lililopita jijini Dar es Salaam na baadaye kupigwa jijini Mwanza huku nguli wa muziki wa dansi Koffi Antonio Olomide akiongoza mashambulizi. Leo ni zamu ya jiji la Mbeya ambao watapata burudani kali kutoka kwa Mapacha wa tatu na kundi la Extra Bongo chini ya Ali Choki.
Kijana wa Mjini Moshi, ambaye anakula maisha jijini Dar es Salaam, akiwa na kundi la Twanga Pepeta, Mkaanga Chips, Martin 'Kibosho' Shao, akiwajibika katika idara yake ndani ya Tamasha la Tusker Carnival.
Wacheza show wa Twanga Pepeta wakionesha manjonjo yao katika onesho hilo.
Wasanii wa bendi ya Diamond Musica wakiwa jukwani wakianza kulishambulia jukwa hilo katika tamasha hilo. |
Wasanii wa bendi ya Diamond Musica wakilishambulia jukwani wakati wa tamasha hilo. |
Wadau wakikata kinywaji wakati wa tamasha hilo la Tusker Carnival, mjini Moshi. |
Wadau kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti tawi la Mjini Moshi nao, walikuwepo ndani ya Viwanja vya Ushirika Mjini Moshi katika tamasha hilo la Tusker Carnival.
Wadau wakila Bata huku wakishushia na bia ya Tusker Baridi. Kwakweli ilikuwa ni burudani na makulaji katika tamasha la Tusker Carnival.
Wadau wa Mjini Moshi, nao walikuwepo uwanjanai hapo.
Watu wakizirudi ngoma katika tamasha hilo.
Huyu anajulikama kama Baloteli wa Bongo au Mbuyi Twitwe wa Twanga Pepeta, akifanya vituko vyake katika jukwaa la Tusker Carnival mjini Moshi.
Palikuwa hapatoshi Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi, watu nyomi wakifuatilia burudani kutoka tamasha la Tusker Carnival. (Picha kwa hisani ya Father Kidevu Blog)
No comments:
Post a Comment