TANGAZO


Friday, December 21, 2012

Mkutano wa CCM Mbeya wafana licha ya kutawaliwa na ushabiki wa Kisiasa, Mbunge Sugu awatuliza wafuasi wake wasilete fujo kwenye mkutano huo



Baadhi ya wananchi na wapenzi wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini wakiwa katika mkutao huo uliyofanika katika kiwanja cha Kabwe Mwanjelwa.

Mashabiki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa na bango linalokipongeza chama hicho katika mkutano huo.

 

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mulugo akiongea na wananchi na wapenzi wa CCM, huku akielezea sera za Chama chake Cha  Mapinduzi (CCM) na mikakati yake.

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi(Mb), akiwasalimia na kuwahutubia wananchi na wana-CCM wa Mbeya Mjini katika mkutano huo  jana.


Mashabiki wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa chama hicho, walikuwepo mkutanoni hapo jana.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM, mkoani humo wakiwa kwenye mkutano huo.
 
Wanachama wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
 
Viongozi wa CCM, wakionesha hamasa ya chama chao, kwenye mkutano huo.
 
Baadhi ya wanachama wa CCM mkoani humo wakishangilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi wao kwenye mkutano huo.

Vituko vilianza hapa,  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Norman Sigalla akipokewa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHDEMA), upande wa pili wa barabara kuu iendayo Tunduma.

Mashabiki wa Chadema wakimshangilia Mkuu wa Wilaya hiyo, huku wakimfuata na kumwambia njoo huku tuna sera nzuri.
Mkuu wa Wilaya huyoo, anatimkia kwenye mkutano wao wa CCM.
Mkuu wa Wilaya, anavuka barabara kuelekea mkutanoni baada ya kuwaacha hoi washabiki wa Chadema.
 
Ngoma inogile, sasa naye Mbunge wa Mbeya Mjini, Mr II, 'Sugu' anapita barabarani,  wafuasi wa chama chake cha  Chadema wanamzuia, ashuke hapo kwenye mkutano wa CCM.
Kazi kweli kweli, ushabiki wa kisiasa hapa barabara imefungwa kwa muda kupisha shamra shamra hizo.
Mashabiki wa Chadema wamzuia kabisa Mbunge Sugu, asipite na ashuke eneo hilo.
Hakika Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ameshuka kwa hasira toka katika gari lake ili aongee na wafuasi wa Chadema.

Mashabiki hao wakiweka amani ili Mbunge Sugu aweze kuongea nao.
Mbunge Sugu, akiwasihi na kuwaomba wapenzi na mashabiki wa Chadema, watulie na wawaache CCM, wafanye mkutano wao, kwa amani na kuwataka kuwa wastaarabu kwa kwa suala hilo, huku akishangiliwa.
Mbunge Sugu akizungumza nao.
"Sasa naombeni njia nirudi zangu home, kwani nimechoka, nimetoka katika kikao, wapendwa acheni fujo, naombeni niachieni njia niende", aliwaomba Sugu.
Jamaa wamekubali, wamemwachia njia, Sugu akaondoka.
Sugu huyooo anaenda zake.
Matukio yote haya yametokea jana katika kiwanja cha Kabwe jijini Mbeya. (Picha zote na Mdau wetu)

No comments:

Post a Comment