TANGAZO


Wednesday, December 26, 2012

Tusker yaikandamiza Yanga bao 1-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Wachezaji wa timu za Tusker ya Kenya na Yanga ya jijini Dar es Salaam, wakiingia Uwanja wa Taifa, kwa ajili ya mpambano wao wa kirafiki uwanjani hapo leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mchezaji Joseph Shikokoti wa Tusker ya Kenya, akipiga mpira kichwa huku akizongwa na George Banda wa Yanga katika mchezo huo wa Kirafiki wa Kimataifa, Uwanja wa Taifa, Dar es salaam leo. Katika mchezo huo, Yanga ilikubali kichapo cha bao 1-0.

Mchezaji Joseph Shikokoti wa Tusker ya Kenya, akiwa ameanguka chini huku David Luhende wa Yanga akijaribu kumtoka katika mchezo huo wa Kirafiki wa Kimataifa, Uwanja wa Taifa, Dar es salaam leo.
 
 George Banda wa Yanga, akimtoka Humphrey Okoth wa Tusker wakati wa mchezo huo.

 George Banda wa Yanga na Humphrey Okoth wa Tusker wakikimbilia mpira wakati wa mchezo huo.

 Humphrey Okoth wa Tusker, akiondoa mpira miguuni mwa David Luhende wa Yanga.

 David Luhende wa Yanga (kulia), akiwania mpira wa kichwa na Luke Ochieng wa Tusker ya Kenya.

 Said Bahanuzi wa Yanga, akijaribu kumhadaa Joseph Shikokoti wa Tusker wakati wa mchezo huo.

Said Bahanuzi wa Yanga, akijaribu kumtoka Joseph Shikokoti wa Tusker, ambaye naye anawania kuuondoa mpira miguuni mwa mchezaji huyo.

Mashabiki na wanachama wa Yanga, wakifuatilia mchezo huo, wakiwa wameshika tama baada ya timu yao kukubali kufungwa goli moja na Tusker hadi wakati huo.

 Mashabiki na wanachama wa Yanga, wakifuatilia mchezo huo, wakiwa na huzuni kubwa bada ya timu yao kukubali kichapo cha bao 1-0. 

Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukisomeka Yanga 0 na Tusker ya Kenya 1.
 
 Kabange Twite wa Yanga, akikimbiza mpira na Jesse Were wa Tusker.

Golikipa wa Yanga, Ally Mustafa, akidaka mpira huku akifuatwa na Jesse Were (kulia) wa Tusker na Stephano Mwasika wa timu hiyo. 

No comments:

Post a Comment